Habari za Punde

Wanafunzi waliopata mshtuko wa mabomu walazwa Hospitali ya Chakechake

 BAADHI ya Wanafunzi wa skuli ya Sekondari Madungu na Shamiani Chake Chake Pemba, wakiwa nje ya hospitali baada ya kurudi kuwafariji wanafunzi wenzao tisa, waliopata mshuko wa mabomu yaliyokuwa yakipigwa na vikosi vya ulinzi na Usalama Mkoa wa kusini Pemba, katika maeneo ya mji wa Chake Chake asubuhi ya leo.(Picha Thureya Ghalib, PEMBA.)
 BAADHI ya wanafunzi wakiwa ndani ya hospitali ya chake chake, sehemu ya mapokezi ya wagonjwa baada ya kuiwafikisha wanafunzi wenzao kupatiwa matibabu, kutokana na mshtuko walioupata kufuatia uripuaji wa mabomu yaliyofanywa na vikosi vya ulinsi na usalama Mkoa wa Kusini Pemba, katika maeneo mbali mbali ya mji wa chake chake(Picha Thureya Ghalib, PEMBA.)
 BAADHI ya waandishi wa habari kisiwani Pemba, wakifanya mahojiano na baadhi ya wanafunzi walifikishwa hospitali ya Chake Chake baada ya kupata mshtuko ya uripuaji wa mabomu, yaliyofanywa na vikosi vya ulinzi na usalama kisiwani Pemba, katika mji wa chake chake leo asubuhi(Picha Thureya Ghalib, PEMBA.)
MMOJA wa Wanafunzi wa skuli ya Madungu Sekondari waliolazwa katika hospitali ya chake chake baada ya kupata mshtuko wa uripuaji wa mabomu yaliyofanywa na vikosi vya ulinzi na usalama mkoa wa kusini Pemba, katika maeneo mbali mbali ya Mji wa Chake Chake(Picha Thureya Ghalib, PEMBA.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.