Habari za Punde

Yanga Wapanga Safari ya Pemba kujiandaa na Simba

Klabu ya Yanga kama kawaida yake inatarajiwa kuweka kambi kisiwani Pemba kujiandaa na mechi dhidi ya watani wake Simba, Oktoba Mosi.


Pambano hilo tayari limekuwa gumzo kubwa hapa nchini hata kabla ya timu hizo kumaliza mechi zao za wikiendi ijayo.
Taarifa zimeeleza kutoka ndani ya klabu hiyo zimedai kambi ya Pemba imeonekana kuwa na baraka zaidi kwa Yanga ambayo msimu uliopita iliichapa Simba ‘nje ndani’.

“Kila kitu kinaonyesha hivyo, kambi itakuwa Pemba. Lakini ni suala la kusubiri sasa, tutajua nafikiri ndani ya siku mbili,” kilieleza chanzo.

“Hata kocha anavutiwa na kambi ya Pemba pia ushirikiano wa wanachama na mashabiki kule ni mkubwa.”

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.