Na salminJuma -Pemba
Taarifa zinasema kua moto huo ulianza kuwaka tokea juzi majira ya saa 12 za jioni ambapo wananchi waliyojitokeza kuuzima bila ya kutambuakua upo baadhi yao hawakuuzima vizuri na hatimae kuendelea kuwaka mpaka siku ya pili.
Mmoja miongoni mwa wanakijiji hicho ndg: Kassim Juma Abdalla amesema tukio hilo ni la kusikitisha na kwa kukisia mashamba yaliyoteketea kwa moto huo ni mashamba sita.
Amesema mara baada ya kupata taarifa hiyo alikwenda moja kwa moja katika eneo la tukio na kushuhudia uwepo wa moto huo huku ukiendelea kuteketeza mikarafuu iliyokuwamo katika mashamba hayo, hivyo kwa pamoja akiwemo mkuu wa misitu walaya kuuzima ili kunusuru majanga zaidi.
Akijibu suala la mwandishi wa habari hizi aliyetaka kufahamu nani waliyohusika kuuwasha moto huo pamoja na sababu iliyowafanya kufanya hivyo, sheha huyo amesema kuampaka muda huu bado hawajafahamu nani wahusika wala sababu yakufanya hivyo na kwakushirikiana na jeshi la polisi mkoa wanaendelea na uchunguzi ili kubaini halihalisi ya tukio hilo.
Kwa mujibu wa wakadiriaji wa mazao kutoka ZSTC, mikarafuu hiyo kwa mwaka inauwezo wa kuzalisha kilo 1160 sawa na gunia 23 yakiwa na thamani ya shilingi milioni kumi na sita laki mbili na arubaini elfu.
No comments:
Post a Comment