STATE
HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF
THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 25.11.2016

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuzipatia
ushirikiano taasisi zote za dini bila ya ubaguzi kwa kuzingatia misingi ya
Kikatiba na uhuru wa kuabudu kama ilivyoanishwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Hayo yameelezwa na Mke
wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema
Shein wakati alipokuwa na mazungumzo na viongozi na Waumini wa Madhehebu ya dini
ya Kikristo huko katika ukumbi wa Nyumba za Wazee Sebleni.
Katika maelezo yake
Mama Shein, alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Awamu ya Saba chini
ya uongozi wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein inathamini sana mchango wa waumini hao
kwa maendeleo ya ustawi wa jamii.
Alisema kuwa jitihada
za taasisi za madhehebu ya dini zinatambuliwa katika kuungana na Serikali
katika kuwapatia wananchi huduma ambali mbali za kijamii zikiwemo afya na
elimu.
Alieleza kuwa jamii
inatambua na kuthamini sana jitihada za waumini hao za kuhubiri amani hapa
nchini.
Hivyo, Mama Shein
alitoa wito kwa waumini hao wasichoke na waendelee kuilinda amani kwa nguvu zao
zote kwani pasipo amani hakuna maendeleo wana waumini hawawezi hata kumuabudu
Muumba wao.
Aidha, Mama Shein
alieleza kuwa vitendo vya ukatili na udhalilishaji vinavyosababishwa na baadhi
ya watu vinatokana na kuyadharau maamrisho ya Mwenyezi Mungu na kuamua kumfuata
shetani ambaye siku zote huwa anashawishi kufanya mambo maovu.
Pia, Mama Shein
aliwasisitiza waumini hao kuwasimamia watoto na vijana ili wawe makini katika
matumizi ya mitandao ya kijamii sambamba na kujiepusha na madawa ya kulevya na
kutoshiriki katika vitendo vyote vya
kuvunja sheria.
Nae Mke wa Makamo wa
Pili wa Rais wa Zanzibar, Mama Asha Balozi alisisitiza haja ya mashirikiano na
akiahidi kuviunga mkono vikundi vya maendeleo ya akinamama hao.
Mapema Mama Fatma
Karume nae alitumia fursa hiyo kueleza uhusiano wa kihistoria uliokuwepo kati
ya waumini wa dini ya kikristo na dini nyengine hapa nchini huku akiwasisitiza haumini hao kuzidisha
mashirikiano na kuendeleza amani na utulivu uliopo hapa nchini.
Kaimu Naibu Katibu
Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma alitumia fursa hiyo kumpongeza Mama Shein kwa
kukamilisha ziara hizo za shukrani katika Mikoa ya Pemba mnamo Novemba 5 hadi 8
mwaka huu na kuendelea katika Mikoa ya Unguja kuanzia Novemba 21 na kumalizia jana tarehe 24.
Waziri wa Kazi,
Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Maudline Castico aliwaeleza
waumini hao juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali katika kupiga vita
suala la unyanyasaji wa wanawake na watoto na kuahidi kuwa waumini hao
wataendelea kushirikiana na Serikali yao.
Nao Waumini hao walieleza
kusikitishwa na kulaani kwa nguvu zote vitendo vya ubakaji wanavyofanyiwa
watoto na kutaka juhudi zaidi ziendelee kuchukuliwa katika kupiga vita vitendo
hivyo.
Aidha, walitumia fursa
hiyo kueleza mafanikio na changamoto mbali mbali zinazowakabili pamoja na
kueleza matumaini yao kwa kuendelea kumuunga mkono Dk. Shein na kusema kuwa
yeye kuwa Rais wa Zanzibar wanajivunia sana.
Wakati wa mchakato wa
Kampeni za Uchaguzi uliopita Mama Shein alikutana na Waumini hao wa Unguja na
Pemba ambapo aliwanasihi kuliombea taifa ili lizidi kuwa na amani na kuingia
katika mchakato huo kwa salama.
Rajab
Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment