Habari za Punde

Ufunguzi wa Barabara Kitope

Na. Othman Khamis OMPR. 

Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda alitoa tahadhari hiyo wakati wa hafla fupi ya kukabidhi pamoja na kulizindua rasmi Jengo la Maabara ya Skuli ya Sekondari ya Kitope iliyomo ndani ya Wilaya ya Kaskazini “B”.

Balozi Seif  alisema wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Kitope kwa sasa hawana sababu ya kufanya vibaya katika mitihani yao ya Kitaifa kutokana na kumalizika kwa Jengo hilo la Maabara ambalo lilikuwa kilio kwao na walimu wao kwa karibu miaka Kumi sasa.

Aliwaasa Wanafunzi hao kuhakikisha kwamba Vifaa walivyopatiwa kwenye Maabara ya Skuli yao wataendelea kuvitunza kwa tahadhari  ili viweze kudumu kwa kipindi kirefu na kutumiwa pia na wanafunzi wenzao watakaofuatia baada ya wao.

Katika kusaidia kupunguza changamoto zinazowakabili walimu na wanafunzi wa skuli ya sekondari ya Kitope Balozi Seif aliahidi kuwapatia mashine Moja ya Fotokopi na kuuagiza Uongozi wa Skuli hiyo kufanya tathmini ya matengenezo ya vyoo, milango na madirisha kwa Darasa wanaloendelea kulijenga kwenye skuli ili kujuwa gharama zitazohitajika. 

Akisoma risala kwa niaba ya walimu na wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Kitope Mwalimu Wanu Ndende Juma amemuelezea Mwakilishi wa Jimbo liliomo Skuli hiyo Balozi Seif Ali Iddi kuwa anapenda Elimu kiasi kwamba amekuwa mshirika mkubwa katika maendeleo ya skuli ya Kitope.

Wamemshukuru na kumpongeza Balozi Seif  kwa uzalendo wake wa kujikubalisha kuwa Mkombozi katika kuchangia  Sekta ya Elimu uliomuwezesha ndani ya kipindi cha Miezi Mitatu kufanya mambo mengi katika Sekta hiyo kwenye Jimbo analolitumikia la Mahonda.

Mapema Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mheshimiwa Riziki Pemba Juma aliwaomba Wanafunzi wa Skuli hiyo ya Sekondari Kitope kuongeza juhudi katika masomo yao hasa yale ya fani ya Sayansi ili kujitengenezea fursa pana ya kuendelea na masomo yao katika viwango vya Vyuo vya juu.

Mh. Riziki alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali imeanzisha utaratibu maalum wa kutenga nafasi kumi za kufadhili wanafunzi watakaopata Daraja la Kwanza kwenye Mitihani yao ya Kidato cha sita katika Fani ya Sayansi ili waendelee na masomo yao katika kiwango cha  Digirii ya kwanza.

Jengo hilo aliloligharamia yeye pamoja na kupata msaada wa nguvu za ufadhili wa baadhi ya vifaa kutoka Ubalozi wa Jamuhuri ya Watu wa China na Kampuni ya mitandao ya simu za mkononi ya Tigo limegharimu jumla ya shilingi za Kitanzania Milioni 38,780,000/-.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.