Habari za Punde

Wafanyabiashara watakiwa kuwa makini na vitendo vya utapeli

Jeshi la polisi mkao wa Mjini Magharibi limewatajka wananachi hususan wafanya biashara hususan wafanya biashara kuwa makini na wimbi la vitendo vya utapeli vilivyoshamiri katika siku za karibuni. 

Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Hassan Nassir ametowa rai hiyo kufuatia polisi kufanikiwa kuwakamnata watu wawili waliojipatia kiasi cha shilingi 31 milioni baada ya kufanya manunuzi na kutowa hundi bandia katika mitaa ya Amani na Mbuyuni. 

Amewataja watu hao kuwa ni Festo Kayange Masanja mkaazi wa Migombani na Othman Mohamed Suleiman mkaazi wa Kwarara 

Kamanda Hassan ameeleza pia kwamba Polisi imefanikiwa kukamata katuni kumi na nane za bidhaa ambazo tayari zilishachukuliwa kitapeli na watu hao. 

Katika hatua nyengine Jeshi la Polisi limegundua vituo sita vinavyotengeneza vyeti na vitambulisho bandia ikiwemo leseni, bima na vyeti vya kuzaliwa na linakusudia kufanya operesheni kubwa kudhibiti hali hiyo.

Source: ZBC

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.