Habari za Punde

Wajasiriamali wa Kikundi cha Kusokota Kamba Kisiwani Pemba.

Wajasiriamali wa Kikundi cha Ushirika cha Kazi ni Uhai cha Ungi Msuka Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba,  kinachojishuhulisha na utengenezaji wa kamba za Usumba, kwa kutumia makumbi wanayoyafukia chini ya bahari kwa muda wa mwaka mmoja, waki chambua usumba mzuri kwa lengo la kutengeneza kamba, kamba ambayo kilo huuzwa shilingi Elfu Tatu (3000).
Mwenyekiti wa Kikundi cha Ushirika cha Kazi ni Uhai, cha Ungi Msuka Pemba Ndg Hamad Juma Masoud, akitowa mafunzo kwa wanakikundi hao jinsi ya kusokota kamba kwa kutumia mashine ya kienyeji ya mbao akitowa maelekezo hayo kwa wanakikundi hicho.  
Mwenyekiti wa kikundi cha Kazi ni Uhai, cha ungi Msuka kinachojishuhulisha na Utengenezaji wa kamba ya Usumba, Hamad Juma Massoud, Akisokota kamba hiyo kwa kutumia mashine maalumu ya mbao,kamba hiyo kilo inauzwa shilingi Elif Tatu, (3000). (Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.