Habari za Punde

Wambaa wafurahia kupatikana maji

Na Salmin Juma kutoka Pemba

Wananchi wa Wambaa wilaya ya Mkoani mkoa wa kusini Pemba wameanza kufurahia upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama vijijini mwao baada ya kuteseka kwa muda wa miaka isiyopungua 30 ya kutopata huduma hiyo.

Wamesema tatizo la maji vijijini kwao lilikua nia la muda mrefu kiasi ya kwamba walishakata tamaa juu ya upatikani wa huduma hiyo hali ambayo iliwapelekea kuishi kwa shida ukizingatia kua maji ndio hitaji kubwa katika maisha ya mwanaadamu.

Kufuatia kuwepo kwa tatizo hilo muda mrefu katika vijiji Mitakawani na Mibaleni Andikoni Wambaa taasisi ya kiisilamu ya Istiqama kusini Pemba iliguswa na mkasa huo na hatimae kuanza mchakato wa kutafuta suluhisho la tatizo hilo na sasa huduma hiyo imeanza kupatikana bila ya usumbufu.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mitakawani katika ziara maalum ya ukaguzi na ufunguzi wa huduma hizo mkuu wa huduma za jamii kutoka jumuiya ya Istiqama kusini Pemba Fadhilat Sheikh Khalfan Bin Sleiman Tiwany amesema, amefurahishwa kuona huduma hiyo sasa inapatikana kiurahisi tofauti na hali ilivyokua awali.

Amesema mara baada ya kusikia tatizo hilo linalowasakili waisilamu wenzake aliamua kulivalia njuga kupitia taasisi yake kulitatua na hatimae wamefanikiwa "tushukuru kwa hatua tuliyofikia, nawaomba tuitunze mbiundombinu hii ili izidi kua endelevu na shida hii isurudi tena vijijini kwetu" alisema shekh Khalfan.

Mmoja miongoni mwa wanakijiji hicho Bi Khadija Juma Ali ameipongeza taasisi ya Istiqama kwa kuwafikishia huduma hiyo karibu na makaazi yao ambapo amesema awali walipatashida kuisaka huduma hiyo kiasi ambacho hawakua na raha katika maisha.

"kwakweli tulikua tunateseka sana, tatizo hili lilikuwepo tokea hatujazaliwa mpaka leo hii, tulikua tunakwenda mbali sana tena kwa madau, tunakwenda kuteka maji kijiji chengine, hapa sote tumefanya hijabu na meno kuuma kwa ndoo za maji" alisema Bi Khadija.

Nae Halima Othman Hamad amesema tatizo la maji kijijini kwao lilidumu takraban miaka 30, hali iliyowafanya hasa wanawake kua wabobu wa miguu kutokana na umbali wa masafa ya kwenda kutafuta huduma hiyo.

"muda mwengine hulazimika kujitwika ndoo mbili kichwani ili tusisumbuke kurudi tena" alisema Bi Halima.

Kwa upande wa wanakijiji cha Mibeleni Andikoni ambao pia walikua ni wahanga wa huduma hiyo pia wameonesha kufurahishwa na upatikanaji wa huduma hiyo kijijini kwao huku wakisema kua waliteseka muda mrefu kupata huduma hiyo.

Nao Sheha Faki Kombo mkaazi wa kijiji hicho amesema, alau sasa wanaiona nafuu katika huduma hiyo tofauti na hali ilivyokua awali.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu sheha wa Jumla ya mifereje tisa ya maji imesambazwa katika vijiji tofauti vya Wambaa kutoka katika njia kuu ya maji ya serikali ambapo awali maji yalipatikana katika masafa marefu na ilichukua kiasi ya masaa mawili kufuataji huduma hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.