Habari za Punde

Wanafunzi wanaomaliza mitihani ya Taifa nchini watakiwa kujiepusha na matendo maovu


Na Salmin Juma, Pemba  

Vijana wanaomaliza kufanya mitihani yao inayoendelea kitaifa ya darasa la kumi na mbili na kumi wametakiwa kujiweka mbali na matendo maovu kwakuwa wako katika kumuomba Mwenyezi Mungu kuwasaidia kuipasi mitihani yao. 

Hayo yamesemwa na wanajamii kwa nyakati tofauti katika kuwapa nasaha vijana hao, kujiepusha na kujitumbukiza katika matendo maovu mara tu watakapomaliza mitihani wakiamini kuwa kilichobaki ni kujivinjari katika maeneo mbali mbali ya starehe huku wakisubiri matokeo. 

 Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mmoja kati ya wazazi na mlezi wa vijana kutoka shehia ya wawi, Abdallah Miraji Abdallah ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya wadhamini ya skuli ya kislamu ya Alhuda iliyopo Makungeni Wawi amesema wanafunzi kabla ya mitihani yao wanatuma maombi mbalimbali miskitini kuombewa dua ili kuipasi mitihani hio, ila cha kushangaza mara baada ya kumaliza kuifanya hata kabla ya matokeo wanafunzi hao huwa tayari wanafanya masherehe mbali mbali ya kumuasi Mwenyezi Mungu kwa madai kuwa eti wanaagana. 

Kwa upande wake Rais mstaafu wa skuli ya DK.Omar Ali Juma wawi Nd;Fahmiy Talhat Abdullah amesema ni jambo la kusikitisha mno kuwaona vijana wengi mara baada ya kumaliza mitihani yao huelekea kwa wingi katika safari za ufukweni na maeneo mbali mbali ya starehe na huko hufanyika matendo ya kumuasi Mwenyezi Mungu jambo ambalo amesema kamwe, kwa matendo hayo wasifikiri kuwa wanaweza kupata huruma kutoka kwa Mungu juu ya kile wanachokiomba. 

Aidha amewataka wazazi na walezi pamoja na walimu kuliona hilo kuwa ni tatizo na kuwakanya watoto wao na wanafunzi wao kutokushiriki katika matendo hayo ya kumuasi M/Mungu kwani amesema hayatowapeleka mbele bali kuwarudisha nyuma.

 Imekuwa ni kawaida kwa wanafunzi nchini kila inapofikia kipindi kama hiki cha kumalizia mitihani yao kujitokeza na kuungana pamoja katika fukwe mbali mbali za bahari huku wakisingizia kuagana na ndani yake hujitokeza matendo yasiyofaa miongoni mwao kama vile zinaa, kunywa pombe, na mengineyo. 

Kwa upande wake sheha wa shehia ya Mizingani wilaya ya mkoani mkoa wa kusini Pemba bw;Rajab Mbwana Rashid amesma: "Ilimu ni muhimu kwa wakati tulionao, na ulimwengu tulionao ni tofauti na wazamani, cha msingi vijaa ni kukaa pamoja, kushirikiana na kuachana na mambo ya starehe, pombe, madawa ya kulevya na anasa bado haujafika wakati wao kuyafanya hayo" alisema sheha huyo. 

Pia amewataka wanafunzi wanapomaliza mitihani yao, wasikimbilie katika kumuasi Mungu bali watafakari kwa kina huku wakizidisha maombi ili wafanyiwe wepesi katika matokeo yao. 

Ni kawaida kwa baadhi ya wanafunzi wengi nchini Zanzibar na Tanzania kwa ujumla wanafunzi kabla ya kuanza mitihani ya taifa kufikisha maombi katika nyumba za ibada ili watakiwe dua ya mafanikio lakini mara tu wanapomaliza hushuhudiwa katika maeneo mbalimbali ya starehe ikiwamo katika fukwe za bahari na kwengineko, eti wanakuita pikniki au dayout kujivinjari na kuagana na kuhitimisha machofu ya muda mrefu,hivyo wanaaswa kuachana na vitu hivyo kwakua havina tija kwa maslahi yao wala jamii iliyowazunguka.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.