Habari za Punde

Kituo cha Huduma za Sheria Chawanoa Wasaidizi Wake Kutatua Migogoro Katika Jamii.

Na Salmin Juma ,Pemba
Katika muendelezo wa kutatua migogoro na changamoto mbalimbali zinazoikumba jamii ya Pemba katika maswala ya kisheria, Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC) upande wa Pemba kimezidi kuwanoa waajiri wake ambao ni wasaidizi wa sheria (parallegals) wa majimbo yote Pemba kwa kuwakumbushia sheria mbalimbali zinazotakiwa kutiiwa nchini ambazo zinagusana karibu na majukumu yao.

Hayo yamebainika jana katika Mkutano maalum uliyokusudia kutoa mafunzo kwa wasaidizi hao huko Wesha katika Hoteli ya Misali mkoa wa kusini Pemba.

Akifungua mafunzo hayo Mratibu wa kituo hicho Pemba Bi Fatma Khamis Hemed amewataka wasaidizi hao kuwa makini zaidi kwa kile wanacho someshwa, lengo hasa ni kuwapatia elimu juu ya uelewa wa sheria mbalimbali ambazo kwa namna moja ama nyengine zinauhusiano wa karibu na kazi walizopangiwa kuzifanya.

Akiwasilisha mada ya Ufafanuzi wa sheria za Tawala za mikoa sheria nambari 08 /2016 Afisa mipango wa kituo hicho Bw: Khalfan Amuor Mohammed amesema lengo la sheria hiyo kwa serikali ni kukuza kipato cha wananchi na kuondosha umasikini hivyo kwa makusudi serikali imeona ni vyema kupitisha sheria hiyo kwakua katika ngazi za mikoa kujia chini ndiko kwenye umuhimu zaidi.

Muhammed amewataka wasaidizi hao kufahamu kua sheria hiyo moja kwa moja inampa mamlaka waziri husika wa kuweza kugawa mipaka au maeneo ya nchini kwa kushauriana na mkuu wa mkoa husika ikiwa wameona kuna haja ya kimsingi kufanya hivyo.

“ mukiona vile mipaka na maeneo kukatwa basi mujue inafanyika vile kwa mujibu wa sheria ndio iliyompa mamlaka waziri, hilo mulifahamu” alisema Muhammed
Katika sheria hiyo Muhammed amebainisha kazi za mkuu wa mkoa pamoja na mkuu wa wilaya kwa lengo la kuwaongezea taaluma wasaidizi hao ili kuzidisha ufanisi katika kazi zao.

Akiwasilisha mada ya ufafanuzi wa sheria ya usajili wa vizazi na vifo sheria nambari 10 / 2006 bw: Muhammed Ali Maalim kutoka Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara maalum za Zanzibar (idara ya vizazi na vifo) amewataka wasaidizi wa sheria kufahamu kua mototo anapozaliwa anatakiwa kutambulishwa katika mamlaka ya vizazi na vifo ili kupatiwa haki zake za msingi ikiwemo cheti cha kuzaliwa, lakini hivyohiyo mtu kufariki inatakiwa kuwasilisha taarifa zake, amesema hiyo ni kwa mujibu wa sheria na kutofanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria wenyewe.

“ ingawa sheria hii ipo lakini hapa panashida, wananchi wengi hutoa taarifa za kuzaliwa kwa mototo lakini inapotokea mtu kufariki hupuuza kuleta taarifa na wanasahau kua taarifa hizo ndizo zinazoiwezesha serikali kufanya tathmini juu ya sababu za vifo nchini na kama ni maradhi serikali ipate kujipanga zaidi” alisema Maalim.

Maalim ametumia nafasi hiyo kuwashauri vijana nchini hasa wale wanaotaka kujiunga na vikosi vya ulinzi kwakua mara nyingi vikosi hivyo huhitaji umri maalum, imegundulika wapo baadhi ya vijana huchakachua vyeti vya kuzaliwa ili kukidhi matakwa ya mashrti hayo, amesema kunya hivyo ni kosa kisheria na ikigundulika mtu anaweza kuingia hatiani kujibu kosa hilo na sheria inaweza kumbana.

Katika mafunzo hayo pia mada ya sheria ya mototo nambari 6/2011 ilipata nafasi ya kuwasilishwa na mratibu wa kituo hicho bi Fatma Khamis Hemed na Bw: Hassan Abdalla Rashid mwanasheria kutoka Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara maalum za Zanzibar aliwasilisha mada ya sheria ya mamlaka ya serikali za mitaa ya 2014, ambapo mafunzo hayo yataendelea kesho.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.