STATE HOUSE
ZANZIBAR
OFFICE OF THE
PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 1.12.2016
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
leo amemuapisha Mkusa Issac Sepetu, kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya
Zanzibar.
Hafla ya kumuapishwa kwa Kaimu Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya
Zanzibar ilifanyika Ikulu Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali
wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Miongoni mwa viongozi waliohudhuria hafla
hiyo ni Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali
Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar
Othman Makungu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Issa Haji Gavu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi
wa Umma na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman.
Wengine ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh
Saleh Omar Kabih, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed
Mahmoud, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mzee Ali Haji, Meya wa Manispaa ya
Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib pamoja na Washauri wa Rais wa Zanzibar
na viongozi wengine wa Serikali.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address:
2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment