Habari za Punde

Ugonjwa wa Kifua kikuu bado ni tishio, wananchi waagizwa kujitokeza kupima afya zao

Na Salmin Juma, Pemba

AFISA Kifua Kiuu, Ukoma na Ukimwi Kisiwani Pemba, Dk Hasnuu Fakih Hassan, amewataka wananchi Kisiwani hapa kutambua kuwa ugonjwa wa kifua kikuu bado upo, hiyo wanapaswa kujitokeza kupima afya zao mapema.

Wito huo ameutoa huko dodo Pujini Wilaya ya Chake Chake, wakati wa utoaji wa elimu kwa jamii juu ya ungonjwa huo, kutokana na eneo hilo ni miongoni mwa maeneo moja wapo yanayotoa wagonjwa wengi wa TB.

Dk Hasnuu alisema mikakati ya serikali ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 Zanzibar kuwe hakuna hata mgonjwa mmoja wapo anaeuguwa ugongwa huo.

Alisema lengo la utoaji wa elimu hiyo ya kifua kikuu, Ukoma na Ukimwi kwa wananchi wa Dodo Pujini, ni moja ya maeneo yanayotoa wagonjwa wengi wa TB.

“Wananchi wanapoona dalili kifua kuuma sana, kifua kubana, kutokuweza kula, homa za mara kwa mara, mwili kuchoka sana, kutapika damu, kukohoa damu kufika katika vituo vya afya ili kupatiwa matibabu”alisema.

Alisema katika utoaji wa elimu hiyo zaidi ya wananchi 29 wamejitokeza na kuwataka kuwa mabalozi wa wenzao kwa kuwapatia taaluma hiyo, huku mikakati yao ni kutoa elimu ya Afya Uwandani, Tundauwa, Kilindi, Michenzani, Mkoani, Chokocho, malengo yao ni kuibuwa wagonjwa wa kifua kikuu mapema na kuwatibu na kumalizika, ili ikifika 2030 Zanzibar tatizo la kifua kikuu liwelimamalizika.

Akizungumzia hali kwa sasa ya Ugonjwa huo, alisema inatisha tisha kidogo kwani kesi za kifua zipo na zinaendelea kuwepo, mwaka jana wagonjwa 70 kusini na kaskazini waligundulika kuwa na Kifua Kikuu.

Hata hivyo alisema tayari wameshaanza kufanya utafiti kwa maeneo mbali mbali ya Pemba, ili kujuwa watu wenye ugonjwa huo na kuweza kutibiwa mapema, aliwataka wananchi wanapoona dalili za kifua kikuu, kufika katika kituo cha afya kuweza kutibiwa kwani matibabu yake ni bure.

Mratib wa Jumuiya ya Kuelimisha Athari za Madawa ya Kulevya, Ukimwi na Mimba katika umri mdogo (JUKAMKUM) Kisiwani Pemba, Hafidhi Abdi Saidi, amewataka wananchi kuhakikisha wanapima afya zao kwani maradhi ya TB ni hatari na yanatibika pale yatakapowahiwa mapema.

Alisema takuwimu zinaonyesha kuna maeneo maalumu TB inaonekana, hivyo shida yao kubwa ni kuona jamii inakuwa salama katika mambo ya afya.

Hata hivyo aliwataka wananchi kufahamu kwamba TB ipo na nimaradhi hatari zaidi kushinda hata huo Ukimwi, hivyo wanapaswa kwenda katika vituo vya afya wanapoona dalili mapema za kifua kikuu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.