Habari za Punde

Wanawake wa Kikundi cha Solar Makunduchi Kutumia Mapato Yake Kusaidia Jamii Wodi ya Wazazi na Watoto Hospitali ya Makunduchi Zanzibar.

Mwakilishi wa Jimbo la Makunduchi Mhe Haroun Ali Suleiman akikabidhiwa Dawa na Vifaa vyengine na Kiongozi wa Wanawake wa Kikundi cha Solar Makunduchi ikiwa mchango wao kwa Jamii kusaidia Wodi ya Wazazi katika hospitali ya Makunduchi Unguja ikiwa ni pato lao la kuunganisha Umeme wa nguvu ya jua Solar, Mafunzo ya kutengenmeza Umeme wa Jua wameipata Nchini India na kuendeleza utaalam huo kwa kuwaungia wananchi wa kijiji cha makunduchi na vijiji vya jirani kwa harama ndogo. Vifaa hivyo na Dawa vikiwa na gharama ya shilingi milioni moja. Hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya hospitali ya Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja.   
Mwakilishi wea Jimbo la Makunduchi Zanzibar Mhe Haroun Ali Suleiman na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Harusi Said Suleiman wakiwa katika picha ya pamoja na Wanawaki wa Kikundi hicho cha Solar ,Makunduchi. 
Wanawake wa Kikundi cha Solar Makunduchi wakiwa katika wodi ya Wazazi na Watoto wakigawa Maji na Biskuti ikiwa ni mchango wao kwa Jamiii na kuchangia dawa zenye thamani ya shilingi milioni moja kwa Wananchi wa Kijiji cha makunduchi ikiwa ni jitihada zao za elimu waliopata Nchini India ya kutengeneza Umeme kwa kutumia nguvu ya jua Solar. Hutowa huduma hiyo kwa kuwaunganishia umeme wananchi wa makunduchi kwa gharama ndogo ya shilingi elfu sita na kuchangia kila mwezi.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.