Habari za Punde

Balozi Seif Awafariji Wananchi Kisiwani Pemba Walioathirika na Mvua.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwafariji Wananchi wa Kijiji cha Vitongoji ambao nyumba zao zimeathirika la mafuriko ya Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Kisiwani Pemba.
Balozi Seif na Ujumbe wake waliofika Pemba kuangalia athari za Mvua akikagua Nyumba ya Sheha wa Shehia ya Chonga Bwana Yahya Hussein Yussuf iliyoathirika na mafuriko hayo.

Muonekano wa hali ya Msikiti wa Ijumaa wa Kijiji cha Mbuyuni Mkoani Pemba inavyoonekana baada ya kubomoka kutokana na kuangukiwa na kifusi cha Mlima ulipo nyuma ya Msikiti huo.
 Muonekano wa Ghala la Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar {ZSTC} lilivyobomoka kutokana na Mmong’onyoko wa Ardhi hapo Bandarini Mkoani Kisiwani Pemba
Mashamba ya Migomba yaliyopo katika Kijiji cha Changaweni Wilaya ya Mkoani yaliyokumbwa na Upepo mkali na kusababisha kukatika au kung’oka kabisa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na Viongozi wa Serikali na Taasisi za Umma wa Kisiwani  Pemba katika Kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kuwafariji Wananchi wa Pemba Hapo Hoteli ya Achipelaago Chake Chake.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Taasisi za Umma wa Kisiwani  Pemba wakiwa katika Kikao cha majumuisho kilichoongozwa na Balozi Seif kwenye Hoteli ya Achipelaago Chake chake Pemba.(Picha na OMPR)

Na. Othman Khamis OMPR. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itajitahidi kufanya jitihada za ziada katika kuona Wananchi walioathirika na mafuriko ya Mvua za Masika wanasaidia kwa kadri hali itakavyoruhusu.

Alisema jitihada hizo zinatokana na janga kubwa lililowakumba Wananchi katika maeneo mbali mbali ya Visiwa vya Zanzibar  baada ya Makaazi yao kukumbwa na mafuriko mengine yakiharibika kabisa.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa katuli hiyo alipofanya ziara ya siku Moja Kisiwani Pemba kujionea hali halisi ya athari ya mavua za Masika zilizopelekea mamia ya Wananchi kukosa makaazi baada ya nyumba zao kubomoka na nyengine kufunikwa na vifusi vya udongo.

Balozi Seif alisema Timu ya Wataalamu na Viongozi Watendaji wa Serikali wamepewa jukumu la kufanya Tathmini kwa kushirikiana na Wakuu wa Mikoa na Wilaya zilizopata maafa ili kujua maeneo na wananchi wanaopaswa kupewa kipaumbela katika kusaidiwa kuanza tena maisha yao kama kawaida.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amefarajika kuona Wananchi walio wengi katika maeneo mbali mbali yaliyoathiriwa na Mvua za masika kuonyesha mshikamano wao kwa kusaidiana katika kipindi hichi cha maafa.

Alisema mwendo huo ulioweka pembeni itikadi za Kisiasa unafaa kuendelezwa katika vipindi vyote yanapotokea maafa au majanga na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuwa pamoja nao katika vipindi vyote.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliyefuatana na Ujumbe mzito wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na wale wa Chama Tawala alitembelea Ghala la kuhifadhi Karafuu la Shirika la Tifa la Biashara Zanzibar { ZSTC} Mkoani kujionena hali halisi iliyojitokeza kwa kubomoka kutokana na mmong’onyoko wa Ardhi.

Balozi Seif aliupongeza Uongozi wa ZSTC kwa uamuzi wake wa kuyawekea Bima Majengo yake jambo ambalo lita9ungiuza gharama za ujenzi mpya wa Jengo hilo linalohifadhi Karafuu zote za Kisiwa cha 9emba kwa ajili ya kusafirishwa nje ya Pemba.

Balozi Seif aliushauri Uongozi huo wa ZSTC kuhakikisha kwamba majengo mapya wanayojenga yanazingatia kiwango kinachokubalika Kitaalamu ili kujie9usha ma maafa yanayoweza kutokea ikiwemo mi9oromoko na Mafuriko ya Mvua.

Maemba Sfisa Mdhamini wa Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar {ZSTC} Pemba Nd. Abdullah Ali Ussi alisema mmong’onyoko wa ardhi uliosababishwa na Mvua kubwa ulifukia Magunia Mia 527  zenye Tani 23.7 za Karafuu kavu zilizokuwa zimehifadhiwa katika Ghala hilo.

Nd, Abdullah alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba kati ya hayo Magunia 518 yenye Tani 23.3 yameweza kuokolewa na hadi sasa Gunia 9 zenye ujazo wa Kilo 405 zikiwa na gharama ya shilingi Milioni 5.6  bado hazijapatikana.

Alisema gharama za kulerejesha tena ghala hilo katika hali yake ya kawaida linahitaji kiasi cha shilingi Milioni 50,000,000/- ambazo zitashughulikiwa na Shirika la Bima linaloendelea na utaratibu wa kufanya thathmini ya hasara hiyo.

Mapemba asubuhi Balozi Seif na ujumbe wake alitembelea Ghala la ZSTC Mkoani, kuangalia nyumba zilizoathirika katika Kijiji cha Mbuyuni pamoja na  Kijiji cha Changaweni kujionea hali halisi ya Miti ilivyoharibika kutokana na upepo mkali uliovuma na kuambatana na Mvua kubwa.

Balozi Seif  pia akaangalia sehemu ya Bara bara iliyokatika  kutokana na mong’onyo katika Kijiji hicho cha Changaweni,  kuwafariji Wananchi wa Kijiji cha Mwambe ambao nyumba zao zipatazo 15 zimeharibika kutokana na Mvua kubwa pamoja na kuifajiri Familia ya Mzee Ramadhan mohamed aliyefiliwa na Mtoto wake aliyeangukiwa na Ukuta wa Madrasa.

Akiwapa pole Wananchi wa Vijiji vya Chonga na Vitongoji Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar lazima itowe msaada katika muda mfupi kulingana na mazingira yaliyojitokeza  ili kuona maisha ya Wananchi wake yanarejea kama kawaida.

Balozi Seif aliwatahadharisha Wananchi kujiepusha na utaratibu wa kupenda kujenga makaazi yao ya kudumu katika maeneo hatarishi kama  vile sehemu za Milima.

Wakitoa shukrani zao Wananchi walioathirika na kadhia hiyo Kisiwani  Pemba  wameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa jitihada inazoendelea kuchukuwa ya kusaidia Wananchi wake wakati wanaoatwa na majanga.

Bwana Othman Abdulrahman Mabrouk wa Kijiji cha Chonga alisema Wananchi walio wengi wamefarajika kwa kiasi kikubwa kiasi kwamba mitihani wanayoipata inapunguza machungu.

Hata hivyo Bwana Abdulrahman kwa niaba ya Wananchi wenzake wameiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kufikiria njia za kuwasaidia mitaji itakayowawezesha kurejesha matumaini yao ya Kimaisha baada ya fursa walizokuwa nazo kuata mitihani ya mafuriko.

Naye Mmoja wa Vijana wa Kijiji hicho Nd. Suleiman Khamis Rashid alisema io haja kwa Serikali kupitia Wizara inayoshughulikia Taaluma kuangalia uwezekano wa kuwapatia mabuku na Vitabu Watoto walioathirika na mafuriko hayo ambao vifaa vyao vyote vimekumbwa na Maji.

Nd. Suleiman alisema kwa sasa wanafunzi wengi licha ya kufungwa kwa skuli kutokana na mafuriko hayo lakini pia wanashindwa  kuendelea na msomo hayo kwa vile hawana vitabu wala mabuku ya kuandikia.

Akizungumza katika Kikao cha majumuisho kilichofanyika katika Hoteli ya Archipelaago Chake chake Pemba wakati wa Usiku Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  aliwaasa Wasimamizi wa Taasisi za Umma kuhakikisha kwamba kero zinazowakumba Wananchi katika maeneo yao wanazichukulia hatua zinazofaa.

Balozi Seif alisema yapo malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya Wananchi wakiwalaumu Viongozi wa Taasisi kushindwa kuchukuwa hatua kwa wakati na matokeo yake wanajikuta kupata hasara kutokana na uzembe wa Viongozi hao.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alivipongeza Vikosi vya Ulinzi Kisiwani Pemba kwa umakini na umahiri waliouonyesha katika kuwasaidia Wananchi mbali mbali wakati walipokumbwa na maafa hayo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.