Habari za Punde

Kikosi cha KMKM Zanzibar Chafanikiwa Kuuokoa Mwili wa Marehemu Abass Anasi Haji Aliyezama Katika Bonge Mzungu Zanzibar.

Askari wa Kikosi cha KMKM Zanzibar wakiokoa mwili wa Mwananchi Abass Anasi Haji aliyepata ajali katika barabara ya kibondemzungu Wilaya ya Magharibu Unguja wakati akiwa katika safari yake ya kawaida akielekea katika shughuli zake za kawaida, akielekea katika Kijiji cha Fuoni Kibondeni na mauti kumkuta katika eneo hilo akiwa na vespa yaka akikatisha katika barabara hiyo iliokuwa imefunikwa na maji yaliojaa katika bonde hilo na kuvuka barabara hiyo alikuwa akitembea huku akikokota vesopa yake na kupisha gari ndipo alipoteleza na kuingia katika bonde hilo na kuchukuliwa na maji kwenda upande wa pili wa bonde hilo. 
Wananchi na Askari wa Kikosi cha KMKM wakisaidiana kuutowa mwili wa marehemu Abass Anasi Haji baada ya kuzama katika Bonde hilo na mauti kumkuta. Kikosi cha Askari wa KMKM walifanikiwa kuuokoa mwili huo baada ya kuzamia katika bonde hilo hutumika kwa kilimo cha mpunga kwa wananchi wa maeneo ya jumbi na fuoni Zanzibar.
Mwili wa Marehemu Abass Anasi Haji ambaye ni Askari Polisi Kitengo cha Picha Makao Makuu ya Polisi Zanzibar ukipakiwa katika gari la Polisi kwa uchunguzi zaidi katika hospitali ya Mnazi Mmmoja Zanzibar. Marehemu mauti yamemkuta wakati akikatisha katika barabara ya jumbi kuelekea kijiji cha kibondeni fuoni, Barabara hiyo imejaa maji yaliofurika katika bonde hilo na kukiuka barabara hiyo kuelekea upande wa pili wa bonde hilo.
Wananchi wa maeneo ya Fuoni na Jumbi wakiwa katika eneo la tukio hilo wakiangalia shughuli za uokozi zikiendelea katika eneo la tukio.
Umati wa Wananchi wakiwa na hudhuni kutokana na ajali hiyo ya kuzama Mwananchi kastika bonge mzungu jumbi Wilaya ya Magharibi Unguja na kusababisha kifo chake. 
Eneo la barabara iliotokea ajali ya marehemu Abass Anasi Haji kuteleza na kuanguka na kuchukuliwa na maji wakati akikatika katika barabara hiyo wakati akikokota vespa yake wakati akiipisha gari na kumkuta ajali hiyo baada ya kuteleza na kuanguka na kuchuliwa na maji hadi bondeni humo. Juhudi za Vikosi vya Zimamoto na KMKM vilifanikiwa kuupata mwili huo. 
Askari wa Kikosi cha KMKM Zanzibar wakiondoka eneo la tukio baada ya kumaliza kazi ya uokozi wa mwili wa marehemu Abass Anasi Haji aliyepata ajali katika eneo hilo na kusababisha kifo chake.
Mkuu wa Wilaya ya Magharibi B Ndg Silima Haji Haji akizungumza na waandishi wa habari kutokana na tukio hilo la ajali ya kuzama mwananchi wakati akipita katika barabara hiyo akiwa katika safari zake za kawaida. Na kuwataka wananchi kuwa na tahadhari katika maeneo hatarishi hasav katika kipindi hichi cha mvua za masika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibu Unguja Kamanda Hassan Nasir akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbali waliofika katika eneo la uokoaji wa marehemu Abass Anasi Haji, ambaye ni Askari Polisi wa Kitengo cha Picha Makao Makuu ya Polisi Zanzibar. Na kuwaasa watumiaji wa barabara kuwa waangalifu katika maeneo yaliokuwa na maji ili kuepusha ajali ikizingatiwa katika kipindi hichi cha mvua za masika miundo mbinu mingi imeharibiwa na mvua hizo. 

Wananchi wakipita katika eneo hilo la barabara iliopita katika bonde mzungu baada ya kukamilika zoezi la shughuli za uokozi kumalizika lililofanywa na Vikozi vya Zimamoto na KMKM.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.