Habari za Punde

Mtoni wilaya ya Chake balaa washikana mashati

Na mwandishi wetu

Wananchi wa na wakaazi wa Mtoni, wilaya ya chakechake Mkoa wa kusini Pemba wameitaka mamlaka ya maji Zanzibar ( ZAWA ) kuchukua hatua za haraka ili kutatua mzozo unaoonekana kukua siku hadi siku kutokana na upatikani wa huduma ya wa maji kijijini hapo.

Wito huo umetolewa kutokana na pande mbili kijijini hapo Mtoni juu na Mtoni chini kuanza kushikana mashati baada ya Mtoni juu kuunga maji katika bomba iliyotokea Mtoni juu ambapo kila upande kati yao unajiona uko sahihi.

Hayo yamebainika jana mara baada ya redio istiqaama ilipotembelea kujionea hali halisi ilivyo kijijini hapo na kukutana na baadhi ya wahusika katika mgogoro huo unaoonekana kuanza kuwagawa mapande mawili wakaazi wa kijiji hicho .

Mmoja miongoni mwa wakaazi wa Mtoni juu aliyejitambulisha kwa jina la Ali Juma Khamis alipoulizwa na mwandishi wa habari hizi juu ya kile kinachoonekana kua ni mgogoro baina yao amesema kilichofanyika ni watu wa Mtoni bondeni kuunga maji pasi na kufuata utaratibu waliokubaliana.

Amesema makubaliano ni kwamba watu wa Mtoni bondeni waunge mipira yao ya maji katika sehemu ambayo itawawezesha kupata huduma hiyo pande zote mbili lakini wao kwa makusudi waliamua kuunga sehemu waliyotaka wenyewe na kupelekea kukosekana kwa huduma hiyo katika maeneo ya wakaazi wa Mtoni juaa

Aidha amesema kuwa walikubaliana wakae chini wazungumze ili kuangalia uwezekano wa namna gani ya kuunga mipira ili huduma hiyo iwe inapatikana kote lakini hawakulipa umuhimu jambo hilo na kuamua kufanya wanavyotaka wao.

Khamis amesema wao wapo tayari hata kuchangishana fedha ili kuwasaidia wenzao kwa sharti la kuunga sehemu ambayo itawawezesha wote kupata maji bila ya usumbufu.

Mwananchi mwengine jina lake limehifadhiwa ambae pia ni mkaazi wa mtoni juu amesema tokea wakaazi wa mtoni bondeni kuunga maji sehemu hiyo kumepelekea wao kukosa maji.

Amesem pia kumefikia hatua mbaya ya uharibufu wa kukatwa kwa paipu za maji na watu wasiojuulikana.

Kwa upande wake Bw. Zahoro Is-haka mkaazi wa Mtoni bondeni amesema wao hawakuunga tu kwa nguvu zao bali awali walikwenda kwa sheha wa shehia hiyo ili kutaka ridhaa ya kuunga maji ndipo sheha akawaelekeza waende mamlaka ya maji na mamlaka ilifika sehemu hiyo na kuhakikisha kuwa hakuna tatizo lolote litakalo jitokeza pindipo wataungiwa maji sehemu hiyo na ndipo wakaungiwa .

Kwa upande wake sheha wa shehia ya kichungwani Bi Mafunda Hamad Rubea amesema ni kweli alipokea ombi kutoka kwa wakaazi wa Mtoni bondeni la kutaka kuunga maji ambapo alipowataka waende mamlaka ya maji kwani yeye si mtaalamu wa mambo hayo.

Kwa upande wake afisa uhusiano wa mamlaka hiyo kwa upande wa Pemba Nd, Suleiman Anas Massoud amesema wamelipokea kwa masikitiko makubwa suala la kukatwa paipu za maji na kusema kuwa paipu yeyote badala ya kuungwa na kuanza kutoa maji siyo tena ya mtu binafsi bali ipo chini ya mamlaka hiyo na ni kosa kisherea kukata paipu ya maji na atakae tenda kosa hilo atatakiwa kutumikia kifungo cha miezi sita au faini isiyopungua 200,000 au vyote viwili kwa kifungu cha sheria 4 ya mwaka 2006.

Amesema kuwa kitendo cha watu wa mtoni juu kusema kuwa wakazi wa mtoni bondeni wameunga maji watakavyo wao sio kweli bali maji hayo yaliungwa na mafundi wa mamlaka hiyo kwa kufuata sherea zote stahiki.

Aidha amesema kwa sasa kinachofuatia ni kufika maeneo hayo na kukagua nyumba moja badala ya nyengine ili kuwahakiki wateja wao wote pamoja na kuwafungia mita ambazo zitasaidia kujua nani anapata huduma hiyo na nani hapati.

Amemalizia kwa kuwaomba wananchi kuachana na kuchukua hatua mikononi mwao na badala yake kufika sehemu husika pindi linapotokea tatizo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.