Habari za Punde

Timu ya Chuo cha Utawala wa Umma Zanzibar (IPA) yatinga nusu fainali mashindano ya vyuo vikuu

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Timu ya soka ya Chuo cha Utawala wa Umma Zanzibar (IPA) leo imetinga hatua ya nusu fainali kwenye Mashindano ya Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar baada ya kushinda penalty 1-0 dhidi ya SUMAIT kufuatia mchezo huo kuendelezwa mchana wa leo kwenye dimba la Amaan.

Mchezo huo ni muendelezo kufuatia jana kutoka sare ya 2-2 ndani ya dakika ya 90 katika uwanja wa Fuoni kisha kupigiana mikwaju ya penalti 6 na kutoka sare ya 5-5 kufuatia kila timu kukosa penalti1 na kupata 5.

Pambano likalazimika kulazwa jana na kuendelezwa leo kwa mikwaju ya penalti na iliendelea penalti moja moja kwa kila timu ambapo SUMAIT walikosa na IPA wakapata, hivyo IPA wametinga nusu fainali kwa ushindi wa jumla ya penalti 6-5.

Nusu fainali ya Mashindano hayo zitapigwa kesho majira ya saa 10:00 za jioni katika Viwanja Viwili tofauti.

Katika uwanja wa ZU Tunguu watasukumana kati ya Chuo cha Afya Mbweni dhidi ya IPA, na katika uwanja wa Fuoni ZU mabingwa watetezi watakipiga na ZIFA ambao ni makamo bingwa watetezi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.