Habari za Punde

Kutoka Baraza la Wawakilishi leo

Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum Mhe Said Soud Said akichangia Mswaada wa Dawa za Kulevya uliowasilisha katika Mkutano wa Sita wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar akisisitiza mchango wake akiwa na Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM wakati akichangia katika ukumbi wa mkutano.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakiwa katika ukumbi swa Mkutano wa Baraza wakifuatilia michango ikiwasulishwa na Wajumbe kuchangia Mswada wa Dawa za Kulevya Zanzibar.
Kamishna Mkuu wa Bodi ya Mapato Zanzibar Amour Hamil Bakar akifafanua jambo wakati akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kushoto Mwakilishi wa Jimbo la Jangombe Zanzibar Mhe Abdallah Maulid Diwani na kulia Mwakilishi wa Welezo Zanzibar Mhe. Hassan Hafidh (Diaspora.) wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano. 
MWAKILISHI wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akizungumza na Mwakilishi wa Jimbo la Chukwani Zanzibar Mhe. Mwanaasha Khamis Juma wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano wa Sita wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Waziri wa Mawasiliani Ujenzi na Usafirishaji Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume akisisitiza jambo na Mwakilishi wa Jimbo la Paje Zanzibar Mhe Jaku Hashim Ayoub. No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.