Habari za Punde

Madaktari wa Diaspora wa Jumuiya ya Afya na Elimu Marekani Wakitowa Huduma ya Afya Kwa Wananchi wa Zanzibar Hospitali ya Mnazi Mmoja.

Daktari Bingwa wa Ngozi kutoka Marekani akitowa huduma hiyo kwa mwananchi wa Zanzibar aliyefika kupata huduma hiyo katika hospitali kuu ya mnazi mmoja kupata huduma hiyo Madaktari hao Bingwa kutoka Taasisi ya Afya Elimu ya Marekani Diaspora wameletwa na taasisi hiyo kwa ajili ya kutowa huduma kwa Wananchi wa Zanzibar kwa maradhi mabilmbali yakiwemo Maradhi ya Ngozi, Kisukari, Presha na kugawa miwani ya kusomea na kuonea kwa Wananchi wenye matatizo ya macho, Kambi hiyo imefanyika katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kwa muda wa Siku Tano wanatowa huduma hiyo.  
Wananchi wa Zanzibar wakiwa katika viwanja vya hospitali ya Mnazi Mmoja wakisubiri huduma ya matibabu ya Ngozi yanayotolewa na Madaktari wa Diaspora kwa wananchi hao.
Wananchi wa Zanzibar wakiwa katika viwanja vya hospitali ya Mnazi Mmoja wakisubiri huduma ya matibabu ya Ngozi yanayotolewa na Madaktari wa Diaspora kwa wananchi hao.
Daktari kutoka Diaspora akitowa huduma kwa Mwananchi wa Zanzibar kuhusiana na maradhi ya presha aliyefika kupata huduma hiyo katika Kambi hiyo ya Madaktari wa Diaspora kutoka Marekani. wakiwa Zanzibar kwa siku tano kutowa huduma hiyo kwa Wananchi wa Zanzibar.
Baadhi ya dawa za Presha na Sukari zilizotolewa na Madaktari kutoka Marekani wa Diaspora kwa Wananchi wa Zanzibar. 





No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.