Habari za Punde

Rasmin Vilabu 12 Kushiriki Ligi Kuu ya Zanzibar Vimepatikana.Sasa Kutakuwa na Ligi ONE na TWO, Miembeni City na Charawe Hawamo Ligi Kuu Japo Wamepanda Daraja.

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Viongozi wa vilabu 28 vya Unguja na Pemba wamekutana leo katika ukumbi wa Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba na kuamua timu zitakazoshiriki ligi kuu soka ya kwa msimu wa mwaka 2017-2018 ambapo wameamua timu zilizomaliza nafasi ya 1-6 kwa kila kanda, yani Unguja na Pemba ndizo zitakazocheza ligi kuu wakati huo huo Bingwa atapata nafasi ya kuwakilisha Zanzibar katika Kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika.

Timu 16 kati ya 28 zilizosalia ambazo hazijashuka daraja zitacheza ligi two ambapo Bingwa wa ligi hiyo atapata nafasi ya kuwakilisha Zanzibar kwenye kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Timu hizo 12 zilizofanikiwa kucheza ligi kuu (Ligi 1) msimu mpya wa mwaka 2017-2018 ni JKU, Jang’ombe Boys, Zimamoto, Taifa ya Jang’ombe, Polisi, KMKM kwa upande wa Unguja na Pemba ni Jamhuri, Kizimbani, Mwenge, Okapi, Chipukizi na New Stars.

Kwa upande wa timu 16 zitakazocheza ligi 2 msimu mpya wa mwaka 2017-2018 kati ya hizo 8 za Unguja na 8 za Pemba ambapo za Unguja ni Mafunzo, KVZ, Black Sailors, Chuoni, Kilimani City, Kipanga, Miembeni City na Charawe wakati za Pemba ni Dogomoro, Wawi Star, Shaba, Young Islander, FSC, Hardrock, Chuo Basra na Opek.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.