Habari za Punde

Baba wa Mwinyi: Ujio wa Gardiel Haunipi Homa ya Kukosa Namba Mwanangu Kikosi cha Kwanza Yanga Bali Ndio Utamfanya Mwinyi Apige Kazi Zaidi.

Na: Abubakar Khatib Kisandu.

Baba mzazi na meneja wa Mwinyi Haji Ngwali mlinzi wa kushoto wa klabu ya Yanga Mzee Haji Ngwali amesema hana mashaka na mtoto wake ya kukosa namba katika kikosi cha kwanza kwa timu ya Yanga licha ya kusajiliwa mlinzi mwengine wa kushoto Gadiel Michael aliyejiunga akitokea Azam FC.

Mwinyi ambae ni msimu wake wa tatu tangu ajiunge na Yanga amekuwa na wakati mzuri tangu asajiliwe na timu hiyo ambapo amecheza michezo mingi kuliko mpinzani wake wakati huo Oscar Joshua ambapo kwasasa anampinzani mwengine Gadiel Michael aliyetoka Azam FC baada ya Joshua kuachwa.
               
Mzee Haji amesema anaamini mazoezi ndio kila kitu na mpira ni mchezo wa hadharani si mchezo wa kusifiwa katika Magazeti hivyo muhimu kocha wao ndie anaejua nani atamrizisha na kupelekea kumpanga.

Amesema anajua Mwinyi ametoka Zanzibar kwaajili ya soka tu hivyo anaamini mwanawe atafanya vizuri kama ataendelea kujituma mazoezini na kuendeleza kuwa na nidhamu ya hali ya juu.

“Mimi ndie baba mzazi na meneja wa Mwinyi, najua msimu huu kuna changamoto kubwa kwa mwanangu lakini naamini ataendelea kucheza kikosi cha kwanza Yanga, muhimu kuzidi kujituma mazoezini na pia aendeleze nidhamu, mpira ni mchezo wa hadharani, najua changamoto nyingi na wala asishuhulikie sana taarifa za kwenye mitandao ya kijamii, namtakia kila la kheiri washinde Jumatano dhidi ya Simba”. Alisema Mzee Haji.

Jana Jumapili Yanga walikamilisha michezo yao ya kirafiki huko Kisiwani Pemba baada ya kuifunga Jamhuri bao 1-0 huku Mwinyi Haji akingara sana katika mchezo huo baada ya kufunga bao dakika ya 5 na kuonyesha kiwango cha hali ya juu kabisa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.