Habari za Punde

Kikosi cha Timu ya Zimamoto Yaungana na JKU Kuiwakilisha Zanzibar Katika Michuano ya CAF.

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka ya Zanzibar timu ya Zimamoto imefanikiwa kumaliza ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora kwa kushika nafasi ya pili baada ya kuichapa Kizimbani mabao 8-1 mchezo uliopigwa jana katika uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba.

Kwa matokeo hayo Zimamoto imefikisha alama 28 na kushika nafasi ya pili ambapo Bingwa wa ligi hiyo ni JKU alitangazwa karibu ya wiki moja nyuma.

Bingwa (JKU) na Makamo Bingwa wa ligi hiyo (Zimamoto) watawakilisha Zanzibar katika Mashindano ya Kombe la Klabu Bingwa pamoja na Kombe la Shirikisho Barani Afrika ambapo msimu uliopita waliwakilisha Zimamoto na KVZ ambao wote walitolewa mzunguko wa kwanza.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.