Habari za Punde

Kombe la Mtoano Kuaza Rasmin leo.Timu 16 Zinashiriki Kutoka Madaraja Tafauti Zanzibar.

Na: Abubakar Khatib Kisandu.
MICHUANO ya ligi ya Mtoano inatarajiwa kuanza rasmi leo Jumatatu kwa kupigwa michezo miwili itakayochezwa saa 8:00 za mchana na saa 10:00 za jioni katika uwanja wa Amaan.

Michuano hiyo ambayo imeandaliwa na ZFA wilaya ya mjini inashirikisha timu 16 za madaraja tofauti.

Afisa Habari wa chama hicho Mwajuma Juma amesema timu 16 zitashiriki ligi hiyo na mchezo wa kwanza utachezwa saa 8:00 mchana kati ya Hawai na Urafiki.

Aidha alisema kuwa mchezo mwengine utachezwa saa 10:00 ambao utawakutanisha timu ya Shaba kutoka kisiwani Pemba dhidi ya African Coast.

Alisema kuwa chama chao kimekuwa na kawaida ya kuandaa mashindano hayo kila mwaka kwa madhumuni ya kuzipa mazoezi timu ya kujiandaa na ligi ambapo msimu uliopita Bingwa wa Mashindano hayo timu ya Taifa ya Jang’ombe ambae msimu huu hakushiriki.

Aidha alizitaja timu nyengine zinazoshiriki ligi hiyo ni pamoja na Negro United, Gereji, New King, Polisi Bridge, Mwembemakumbi, Raska Zone City, Kundemba, Elhilal, Black Sailors, Polisi, Ujamaa na Mwembeladu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.