Maalim Mkubwa Ahmed Omar akizungumza na wahitimu wa Mafunzo ya Ualimu katika Mahafali ya nne ya Mafunzo ya Ualimu kupitia Elimu Masafa yaliyofanyika katika ukumbi wa TC Michakaeni. Awali Mratibu wa Mratibu wa Kituo cha Walimu Michakaeni Ndugu Rashidi Juma Khamis
Na Ali Othman
Mratibu
wa idara ya mafunzo ya ualimu Pemba Malim Mkubwa Ahmed Omar Amewasihi wahitimu
wa mafunzo ya ualimu kupitia elimu
masafa kuhakikisha kwamba wanaitumia fursa ya elimu waliyoipata katika vituo
vya walimu (TC) kujiendeleza zaidi katika ngazi nyengine za kitaaluma.
Akizungumza
katika mahafali ya nne ya Mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti kupitia elimu masafa
yaliyofanyika katika ukumbi wa TC Michakaeni Chake Chake Pemba, Malim Mkubwa
amewapongeza wahitimu hao kwa juhudi na uvumilivu wao uliowapelekea kumaliza
mafunzo kwa ufanisi.
“Kazi
hii nikazi kubwa sana, mawimbi yake nimazito, nawapongeza kwa kuweza kuvuka
salama na kwa mafanikio” Amesema Malim Mkubwa.
Mratibu
huyo wa idara ya mafunzo ya ualimu Pemba amewataka wahitimu hao kuonesha
mabadiliko katika utendaji wa kazi zao akiwathibitishia kwamba kwasasa wameiva.
Aidha
Malim Mkubwa amempongeza Mratibu wa
Kituo cha Walimu Michakaeni Ndugu Rashidi Juma Khamis kwa kusimamia ipasavyo
majukumu yake. Akitoa mfano wa majukumu hayo Malim Mkubwa amesema Mratibu huyo
amekua wakwanza kuwasilisha marejesho kila mara yanapohitajika.
Awali
Mratibu wa Kituo cha Walimu Michakaeni Ndugu Rashidi Juma Khamis ametoa takwimu
ya wahitimu ambapo jumla yao ni 64 ikiwa 16 kati yao walisomea lugha, 27
Walisomea sayansi ya jamii na 21 kati yao walisomea sayansi.
Nae
Kaimu Mratibu wa Elimu Masafa Pemba Malim Hemed Said Masoud ameelezea kuridhishwa kwake kutokana
na mwenendo mzima wa mafunzo ya ualimu kupitia elimu masafa na kuahidi kusimamia
ipasavyo wanafunzi waliodahiliwa kuendelea na mafunzo hayo kwa awamu nyengine.
Hii ni
mahafali ya nne ya Wahitimu wa elimu masafa kupitia vituo vya walimu TC, ambapo
jumla ya wanafunzi 64 wamehitimu mafunzo hayo.
Malim
Mkubwa Ahmed Omar akizungumza na wahitimu wa Mafunzo ya Ualimu katika Mahafali
ya nne ya Mafunzo ya Ualimu kupitia Elimu Masafa yaliyofanyika katika ukumbi wa
TC Michakaeni Awali Mratibu wa Mratibu wa Kituo cha Walimu Michakaeni Ndugu
Rashidi Juma Khamis
No comments:
Post a Comment