Habari za Punde

Mahafali ya Shule ya Msingi Eden Jijini Mwanza Yavutia Wengi.

Mahafali ya 11 ya darasa la saba katika shule ya msingi Eden Jijini Mwanza yaliyofanyika hii leo ijumaa Septemba Mosi,2017 shuleni hapo yamefana huku yakihudhuriwa na viongozi mbalimbali taasisi binafsi na serikali.

Mgeni rasmi kwenye mahafali hayo alikuwa Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Kanda ya Ziwa, Yessaya Mwakifulefule ambaye amewaasa wahitimu hao kuzingatia masomo na maadili mema waliyofundishwa shuleni hapo ili yaweze kuwaletea matokeo chanya kwenye masomo yao katika ngazi ya sekondari inayofuata.

Mkurugenzi wa shule hiyo, Joseph Mbabazi amewahimiza wazazi na walezi wa wahitimu hao kuwaendeleza vyema kwa kuwachagulia shule zenye sifa bora kama Eden kwa ajili ya masomo yao ya kidato cha kwanza hadi cha nne.

Meneja wa shule hiyo ya Aden, Charlotte Mbabazi amewashukuru walimu, wazazi pamoja na walezi kwa ushirikiano wao tangu kuanzishwa shule hiyo mwaka 2004 na kwamba matarajio ni wahitimu hao kufanya vizuri kwenye mitihani yao ya mwisho, kama ilivyo ada ya shule hiyo.

Awali akisoma risala ya shule hiyo ya msingi Eden, Mwalimu Elzabert Dastan amebainisha kwaka mwaka 2007 wanafunzi 20 walihitimu na kufaulu wote, mwaka 2008 walihitimu wanafunzi 26 na kufaulu wote, mwaka 2009 walihitimu wanafunzi 38 na kufaulu wote, mwaka 2010 walihitimu wanafunzi 45 na kufaulu wote, mwaka 2011 walihitimu wanafunzi 58 na kufaulu wote.

Pia mwaka 2012 walihitimu wanafunzi 86 na kufaulu wote, mwaka 2013 walihitimu wanafunzi 73 na kufaulu wote, mwaka 2014 walihitimu wanafunzi 49 na kufaulu wote, mwaka 2015 walihitimu wanafunzi 79 na kufaulu wote, mwaka 2016 walihitimu wanafunzi 69 na kufaulu wote na kwamba mwaka huu 2017 wanahitimu wanafunzi 74 na matarajio ni wote kufaulu.

Baadhi ya wahitimu wa shule hiyo, wakiwemo Nasra Kombo, Steven Mapesa, Joseph Maxmilian pamoja na Geogina Japheti wamewashukuru waalimu wao kwa kujitoa kuwafundisha vyema ambapo wamesema wanamatumaini makubwa ya kufaulu katika mtihani wao wa mwisho unaotarajiwa kufanyika Septemba sita na saba mwaka huu.     Meneja wa Shule ya Msingi Eden, Charlotte Mbabazi akizungumza kwenye mahafali hayo.     Mkurugenzi wa shule ya msingi Eden, Joseph Mbabazi akizungumza kwenye mahafali hayo Mgeni Rasmi, Meneja wa LAPF Kanda ya Ziwa, Yessaya Mwakifulefule akizungumza kwenye mahafali hayo. Mwl.Elzabert Dastan akisoma risala ya shule ya msingi Eden. Wahitimu wa darsa la saba shule ya msingi Eden iliyopo Kaangaye Ilemela Jijini Mwanza. Wahitimu wa darsa la saba shule ya msingi Eden iliyopo Kaangaye Ilemela Jijini Mwanza. Viongozi mbalimbali meza kuu. Viongozi mbalimbali meza kuu. Baadhi ya waalimu wa shule za Eden. Wahitimu wakiimba wimbo wa kuwaaga wanafunzi wenzao. Wahitimu wakiimba wimbo wa kuwaaga wanafunzi wenzao. Burudani mbalimbali kwenye mahafali hayo. Burudani mbalimbali kwenye mahafali hayo. Wanafunzi wakiigiza kama maafisa wa usalama wakati wa kuzuia ghasia.
  Mgeni rasmi akimkabidhi zawadi kutoka shule ya msingi Eden baada ya kufanya vyema kwenye masomo yake. Viongozi wa shule ya msingi Eden wakipongezwa na wazazi na walezi wa wanafunzi. Mshereheshaji wa mahafali hayo, Mc.Katumba akifafanua jambo Mahafali ya 11 shule ya msingi Eden Jijini Mwanza yamefana.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.