NA
HAJI NASSOR, PEMBA
JESHI
la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, linamshikilia kijana Zuhura Ahmed Ali (29) mkaazi
wa Jadida wilaya ya Wete, akidaiwa kukutwa na kete 3, 621 zinazodhaniwa kuwa ni
dawa za kulevya.
Mwanamke huyo alikamatwa kiulani kwenye kuzuizi cha barabara
eneo la Mbuaguani Mkoani, wakati alipoteremka kwenye gari ya abiria, iliokuwa
imesheni abiria ili akapandie mbele, ndipo alipoitwa na Polisi aliekuwepo hapo,
kwa lengo la kumsalimiana ingawa alionekana na wasiwasi.
Iliofahamika kuwa, wakati Polisi huyo na mwanamke
wakiendelea kusalimiana kikawaida, alionekana na hofu kubwa na kutetemeka ndipo
alipoitwa na kutii amri, ingawa alitaka kujisaidia na na kutoa kauli za
ubabaifu kama mtu alie usingizini.
Baada ya kudai kutaka kujisaidia mara haja kubwa mara haja ndogo,
ndipo Plisi aliekuwepo zamu, alimtilia mashaka na kumkabidhi kwa mkusanya
mapato mwanamke mwenzake aliekuwepo kwenye kizuizi hicho, na wote kwenda kituo
cha Polisi Mkoani na kufanyiwa upekuzi.
Mara baada ya kufika ndani ya Kituo hicho na kufanyiwa
upekuzi na Polisi wanawake, kijana huyo aliekuwa amevalia shungi kubwa jeusi
alikutikana na hizo kete 3,621 zinazoaminika kuwa ni dawa za kulevya.
Kamanda wa Polisi Mkoa huo Sheihan Mohamed Sheihan, alikiri
kukamatwa kwa mwanamke huyo, na kusema mfuko uliokuwa na dawa hizo,
zinazodhaniwa kuwa ni za kulevya, aliufunga vyema kwenye tumbo lake.
Alisema aliziweka vyema kiasi ambacho hata akienda mbio
haziwezi kutoka na kisha kuzitia ndani ya mkoba na kuzibana vyema kwa shungi
lake kubwa jeusi, alilokuwa amelivaa kwa njia ya kama ya kujistiri.
“Hata askari waliomkamata walipata wasisi kwamba huwenda
hizo kete ni zake, maana hazionyeshi kuwa ni mzigo kapewa na mtu anaemfahamu
ampelekee Jadida Wete, maana ulifungwa vyema”,alisema Kamanda.
Aidha Kamanda huyo wa
Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, aliwaambia waandishi wa habari kuwa, tukio hilo
lililtokea majira ya saa 5:00 asubuhi kwenye kizuizi cha barabara ya Mkoani
Mbuguani.
Alisema tayari mwananmke huyo ameshahojiwa na wanalojina na
mtu aliemtaja kumpa mfuko huo, ambapo wote baada ya taratibu kukamilika
watafikishwa mahakamani.
Kwa upande wake mwanamke huyo Zuhura Ahmed Ali (29) mkaazi
wa Jadida Wete, alisema mfuko huo sio wa kweke na amepewa na mtu njiani
amkamatie bila ya kujua ni mzigo wa aina gani.
Alisema yeye baada ya kupewa hakujua nini kilichokuwemo ndani
yake, na baada ya kukamatwa nao alishangaa kuambiwa kuwa mna dawa za kulevya.
Wakati mtuhumiwa huyo akieleza hayo, Jeshi la Polisi limesema lilishangaa
kuona kuwa mfuko huo mwanamke huyo sio wake, ingawa aliuhifadhi kwenye tumbo
kwa nje na kuufunga na kisha kuuvalia shungi.
Baadhi ya wananchi wa Mkoa wa kusini Pemba,
wamesema lazima Jeshi la Polisi liongeze juhudi za kuyasaka madawa ya kulevya,
kutokana na kushamiria katika siku za hivi karibuni
No comments:
Post a Comment