Habari za Punde

Kikapu Kanda ya Unguja Kutimua Vumbi Jumamosi.

Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Maandalizi ya michuano ya mpira wa kikapu kanda ya 

Unguja yanaendelea vyema huku timu kadhaa 

zikithibitisha kushiriki.

Katibu mkuu wa chama cha mpira wa kikapu Zanzibar (BAZA) Abdull-Rahman Mohamed amesema michuano hiyo wanatarajia kuanza kuunguruma kesho Jumamosi Oktoba 21.
“Maandalizi yanaendelea vizuri na Jumamosi ligi yetu kanda ya Unguja itaanza katika Uwanja wa Maisara, na timu tayari zimeshathibitisha kushiri ligi yetu”. Alisema Abdul rahman.

Timu zilizothibitisha kucheza ligi hiyo kwa upande wa Wanaume ni Polisi, Stone Town, JKU, Cavarios, Afrika Magic, Usolo, Zan Kwerekwe, Mwembetanga Sonic, Renger, New General na kwa upande wa Wanawake zitashiriki timu ya Afrika Magic, Duma, New West, JKU na Mbuyuni.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.