KIONGOZI wa
mbio za mwenge wa uhuru, Amour Ahmad Amour, akisalimiana na Mkuu mpya wa wilaya
ya Chakechake Rashid Hadid, wakati mwenge huo akikabidhiwa ukitokea wilaya ya
Mkoani, ili autembeza wilayani mwake, kwa ufunguzi na uwekaji wa mawe ya msingi
kwa miradi mbali mbali ya kimaendeleo
MMOJA ya
wakimbiza mwenge wa uhuru, akisalimiana na Mkuu mpya wa wilaya ya Chakechake
Rashid Hadid, wakati mwenge huo akikabidhiwa ukitokea wilaya ya Mkoani, ili
autembeze wilayani mwake, kwa ufunguzi na uwekaji wa mawe ya msingi kwa miradi
mbali mbali ya kimaendeleo
KATIBU Tawala
wilaya ya Mkoani Pemba, Miza Hassan Faki katikati), akisoma risala ya wilaya
yake, kwenye hafla ya makabidhiano ya mwenge wa uhuru, kwa ajili ya kutembezwa
wilaya ya Chakechake, hafla hiyo ilifanyika skuli ya Ngwachani
VIONGOZI mbali
mbali wakiogozwa na Mkuu wa wilaya ya Chakechake Rashid Hadid Rashid, wa mwanzo
kulia, wakisikiliza hutuba inayotolewa na Katiba Tawala wilaya ya Mkoani Miza
Hassan Faki, hayupo pichani, kabla ya viongozi hao, kukabidhiwa kwa ajili ya
kutembezwa wilaya ya Chakechake.
MKUU wa wilaya
ya Mkoani Hemed Suleiman Abdulla,
(kulia), akimkabidhi mwenge wa uhuru Mkuu mpya wa wilaya ya Chakechake, Rashid
Hadid Rashid, ili nae autembeze ndani ya wilaya hiyo, baada ya kumaliza mbio hizo
wilaya ya Mkoani
KITUO kipya
cha afya cha daraja la pili, cha Pujini wilaya ya Chaechake kisiwani Pemba,
ambacho tayari kimeshafunguliwa na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Amour
Ahmad Amour, kwenye shamra shamra hizo, wilayani humo.
(Picha na Haji Nassor, Pemba).
No comments:
Post a Comment