KIONGOZI mkuu wa madaktari kutoka China
wanaotoa huduma za matibabu Hospitali ya rufaa ya Mkoa ya Abdulla Mzee Mkoani
Pemba, dk Chen Er Dong, akizungumza kwenye hafla ya kutimia mwaka mmoja wa
hospitali hiyo, tokea kufanyiwa matengenezo makubwa, pamoja na utiaji wa saini
wa makubaliano ya ushirikiano wa hospitali hiyo na ile ya Jiangsu Nanjing, kwa
ajili ya mafunzo ya madaktari wazalendo, (Picha
na Haji Nassor, Pemba).
KIONGOZI mkuu wa madaktari kutoka nchini
China dk Chen Er Dong, akisaini makubaliano ya ushirikiano wa Hospitali ya
rufaa ya Mkoa ya Abdulla Mzee na hospitali ya China ya Jiangsu Nanjing, kwa
ajili ya mafunzo, kwa madaktari wazalendo, hafla iliofanyika jana Mkoani Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
WA pili kulia ni Kiongozi mkuu wa madkatri nane kutoka China, dk Chen Er
Dong, akimkabidhili Mkuu wa wilaya ya Mkoani Hemed Suleiman Abdulla, viti 50
kwa ajili ya hospitali hiyo, ambapo wa mwisho kushoto ni Mganga mkuu wa
hospitali hiyo, dk Haji Mwita Haji na Katiba tawala wilaya ya Mkoani Miza
Hassan Faki, (Picha na HajI Nassor,
Pemba)
BAADHI ya viti 50 vilivyotolewa na timu ya
madaktari nane kutoka China, wanaoendelea kutoa matibabu katika hospitali ya
Mkoa ya Abdulla Mzee, ambapo viti hivyo ni kwa ajili ya hospitali hiyo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MKUU wa wilaya ya Mkoani Pemba, Hemed Suleiman
Abdulla, akisalimiana na kiongozi mkuu wa madaktari waliopo hospitali ya Mkoa
ya Abdulla Mzee, dk Chen Er Dong, muda mfupi, baada kusaini makubaliano ya
ushirikiano kati ya hospitali hiyo na ile ya China ya Jiangsu Ninjing, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MADAKTARI nane kutoka China, wakiwa kwenye
picha ya pamoja, mara baada ya kumalizika kwa hafla ya utilianaji saini juu ya
makubaliano ya ushirikiano kati ya hospitali ya Mkoa ya Abdulla Mzee na
hospitali ya Jiangsu Ninjing kwa ajili ya mafunzo ya kitabibu na madaktari
wazalendo, (Picha na Haji Nassor,
Pemba).
No comments:
Post a Comment