Habari za Punde

Mhe Waziri Mwanjelwa Aipongeza NFRA Kuazisha Mradi wa Kuongeza Uwezo wa Kuhifadhi Mazao Kupitia jenzi wa Vihenge na Maghala Nchini.

Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo mara baada ya kutembelea Ghala la Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Makambako, Mkoani Njombe wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja, Leo Novemba 1, 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza na Wakulima wa Mji wa Makambako, Mkoani Njombe katika ukumbi wa Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Makambako, Mkoani Njombe wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja, Leo Novemba 1, 2017.
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua mahindi yaliyohifadhiwa kwenye Ghala la Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Makambako, Mkoani Njombe wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja, Leo Novemba 1, 2017.
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Wa (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba ya namna ya ununuzi na uhifadhi wa mahindi kwenye Ghala la Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Makambako, Mkoani Njombe wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja, Leo Novemba 1, 2017.

Na Mathias Canal, Njombe

Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa amesifu juhudi za uongozi Wa Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kwa utendaji kazi kwa ubunifu kwa kuanzisha Mradi Wa kuongeza uwezo Wa kuhifadhi Mazao.

Mradi huo utahusisha ujenzi Wa Vihenge vya kisasa, Mghala ya kisasa pamoja na ukarabati Wa Ofisi ambapo baada ya mradi huo kukamilika wakala utakuwa umeongeza uwezo Wa kuhifadhi Shehena ya mahindi ya uzito Wa zaidi ya Tani 250,000 ambapo Vihenge vya kisasa ni 190,000 MT na Maghala 60,000 MT.

Mradi huo unataraji kutekelezwa na kampuni mbili za kandarasi kutoka serikali ya Poland (Feerum na Unia Arab) kwa usimamizi Wa Wakala Wa Majengo Tanzania (TBA) ambapo unataraji kugharimu zaidi ya Bilioni 150 za Kitanzania.

Tayari maandalizi ya awali yameshakamilika ikiwemo Utiwaji saini mikataba, Uchunguzi Wa udongo, Tathmini ya athari ya Mazingira, Pamoja na kutembelea eneo la mpango kazi.

Akizungumza wakati akikagua Ghala la Kuhifadhia mahindi Kanda ya Makambako Mkoani Njombe, Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa alisema kuwa Wakala Wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umefanya kazi kubwa ya ubunifu na kujiongeza kwa ajili ya kuwanufaisha wakulima katika Kanda zote saba ikiwemo ya Makambako-Njombe, Kipawa-Dar es salaam, Dodoma, Shinyanga, Arusha, Songea na Sumbawanga.

Alisema kuwa pamoja na Kanda ya Makambako kupangiwa kununua jumla ya Tani 6500 katika msimu Wa mwaka 2017/2018 ambapo baada ya lengo kukamilika ziliongezwa fedha za ununuzi hivyo kununua jumla ya Tani 8,961.530

Akisoma taarifa ya Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Wa (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba alisema kuwa Kanda ya Makambako ni miongoni kwa Kanda itakayoongezewa uwezo Wa kuhifadhi ambapo tayari kuna kiwanja chenye ukubwa Wa Hekari 2,9965 kilichopo Makambako na Mbozi chenye ukubwa Wa Hekari 53.691.

Alisema Wakala umefanikiwa kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kununua baadhi ya Mazao ya Chakula cha ziada kutoka kwa wakulima, Kutoa Chakula cha ziada kwa waathirika, Kutekeleza mkakati Wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini (MKUKUTA) kwa kutoa bei nzuri kwa wakulima wanaouza Mazao yao kwa NFRA sambamba na utekelezaji Wa malengo ya milenia 2025.

Katika ziara hiyo ya kikazi ya Siku Moja katika Mji Wa Makambako Mkoani Njombe, Naibu Waziri Wa Kilimo pia amekutana na kufanya kikao cha kazi na wafanyakazi Wa Wakala Wa Taifa wa Hifadhi ya chakula Kanda ya Makambako ambapo pamoja na mambo mengine amewasihi kufanya kazi kwa Nidhamu, Weledi, Kujituma, Uvumilivu, Bidii na mshikamano.

Wakati huo huo amefanya mazungumzo na wakulima kutoka Kanda ya Makambako ambapo wakulima hao wamesifu Juhudi za serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais Wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwajali ikiwa ni pamoja na kupunguza Tozo na Ushuru.

Wakulima hao kwa nyakati tofauti wameupongeza Uongozi Wa Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula Kanda ya Makambako kwa kuwashirikisha na kuwajali wakulima katika kila hatua ya ununuzi Wa mazao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.