Habari za Punde

Shirika la Posta Tanzania (TPC) Yazindua Nemba Yake Mpya Jijini Dar

Baadhi ya viongozi wa Idara za Shirika la Posta Tanzania, wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa Nembo mpya ya shirika hilo, jijini Dar es Salaam leo, ambapo Mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Dk. Haruni Kondo (kushoto) akiwa na Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe, wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitendelea katika hafla ya uzinduzi wa Nembo mpya ya shirika hilo, jijini Dar es Salaam leo.
Msanii Mrisho Mpoto (katikati), akiwa na baadhi ya wasanii wa bendi yake ya Mjomba Band wakitumbuiza katika hafla ya uzinduzi wa Nembo mpya ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), jijini Dar es Salaam leo.
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), mh.Elias Kwandikwa (kushoto), akisalimiana na kukaribishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Dk. Haruni Kondo, alipowasili tayari kwa uzinduzi wa Nembo mpya ya shirika hilo, jijini Dar es Salaam leo, ambapo. Wa pili kulia ni Kaimu Postamasta Mkuu wa TPC, Hassan Mwang'ombe, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Elia Madulesi (katikati) na wa pili kushoto ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa TPC, Joseph Ngowi.
Baadhi ya magari mapya ya usafirishaji wa mifuko ya barua na vifurushi, yakiwa tayari kwa uzinduzi katika hafla hiyo.
Baadhi ya Malori ya kubebea mizigo na vifurushi yakiwa katika viwanja vya Posta tayari kwa uzinduzi katika hafla ya uzinduzi wa nembo mpya ya shirika hilo, jijini leo. Pia kulikuwepo na mabasi 3 mapya ya kubebea abiria, mifuko ya barua na vifurushi yatakayotumika kwenye njia ya Makambako-Songea na Masasi-Mtwara katika uzinduzi huo.
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa (kulia), akiteta na kufurahia jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Dk. Haruni Kondo, katika uzinduzi wa Nembo mpya ya Shirika hilo, jijini Dar es Salaam leo.
Kaimu Postamasta Mkuu wa TPC, Hassan Mwang'ombe, akizungumza mbele ya Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa (kulia), wakati akitoa maelezo machache kuhusu Shirika hilo. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa (kulia), kuzindua nembo mpya ya shirika na kutoa hotuba yake.
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Dk. Haruni Kondo (kulia) na Kaimu Postamasta Mkuu wa TPC, Hassan Mwang'ombe (kushoto), wakipiga makofi mara baada ya Naibu waziri kuizindua nembo hiyo (mbele yao), jijini Dar es Salaam leo.
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa (katikati), akimpongeza Kaimu Postamasta Mkuu wa TPC, Hassan Mwang'ombe (kushoto), baada ya kuizindua nembo hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Dk. Haruni Kondo.
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa akilijaribu moja ya mabasi 3 wakati akiyazindua katika hafla hiyo.
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa, akipatiwa maelezo na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Dk. Haruni Kondo, kuhusu magari madogo 5 ya usafirishaji wa mifuko ya barua na vifurushi, katika uzinduzi huo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakiburudika kwa kucheza ngoma za Mjomba Band, katika uzinduzi huo.
Baadhi ya waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari, wakiwa kazini kuchukua matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitendeka katika uzinduzi huo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakifurahia jambo katika uzinduzi huo.
Miongoni mwa wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), waliokuwepo katika uzinduzi wa nembo mpya wakiionesha nembo hiyo, mara baada ya kuzinduliwa na Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa, jijini Dar es Salaam leo.
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa, akitoa hotuba yake katika uzinduzi huo, leo jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Bi. Khadija Khamis Shaaban, akizungumza wakati akimshukuru Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa, kwa hotuba yake aliyoitoa.
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa (wa pili kushoto), akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Dk. Haruni Kondo (kushoto), wakijumuika pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa shirika hilo katika kucheza wimbo maalum wa shirika katika uzinduzi huo. 
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa, akiwapungia wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakati akiwaaga, akiondoka katika hafla hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Dk. Haruni Kondo

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.