Habari za Punde

Oman Air Yakabidhi Tiketi Kwa Washindi wa Bahati Nasibu ya Kuchangia Damu Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud akipokea Tiketi Tatu kwa Washindi wa Bonaza la kuchangia Damu Salama kwa Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi lililofanyika juzi katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Michezani Zanzibar akikabidhiwa na Mwakilishi wa Kampuni ya Ndege ya Oman Air, iliofadhili udhamini wa Washindi wa Bonaza hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud akiwaonesha waandishi wa habari Tiketi za Washindi wa Bonaza la Kuchangia Damu Salama juzi katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Michezani baada ya kuchezeshwa bahati nasibu ya washiriki waliochengia Damu Salama Siku hiyo.

 Mkuu wa mkoa wa mjini magharib unguja Mhe, Ayoub muhaamed mahmod kushirikiana na shirika la ndege la Oman Air wamekabidhi tiketi tatu za kusafiri  kwa washindi wa droo ya bahati nasibu ya kuchangia damu iliyofanyika katika bonanza la uchangijaji wa damu katika mkoa wa mjini magharibi unguja ambalo lilifanyika  mwishoni mwa wiki hii.

 Washindi hao watatu Mohamed mussa Ayoub mkaazi wa chumbuni ,Abdallah Alaw mkazi wa Mwanakwerekwe na Maulia Mwinyi mzee ambaye ni diwani wa Mombasa walipatikana mara baada ya kuchezeshwa kwa droo hiyo  iliyokuwa na watu 543 waliojitokeza kuchangia damu kwa hiari katika bonanza la uchangiaji wa damu salama kisonge mkoa wa mjini unguja.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo maalum ya kuwakabidhi tiketi za kusafiri kwa washindi wa droo hiyo   mkuu wa mkoa wa mjini magharib mhe, Ayoub Mohammed Mahmud amewapongeza washindi hao kwa kufanikiwa kushinda nafasi hiyo ya kuweza kwenda kutembea katika mji mmoja kati ya mji wa Dubai,Oman , Bangkok na Bombay  kwa siku mbili huku gharama za safari ya kwenda kurudi ikigharimiwa na Oman air huku huduma za  malazi na makazi  ziki gharamiwa na ofisi ya mkoa wa mjini magharib unguja.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.