Habari za Punde

Nane Bora Ligi Kuu ya Zanzibar Kuaza Baada ya Michuano ya Kagame Julai 2018.

Na. Mwandishi Wetu.
Nane bora ya ligi kuu ya Zanzibar kuanza baada ya kumaliza kwa Michuano ya Kombe la Kagame.Huku FA Cup kuanza baada ya kumaliza kwa mwezi wa Ramadhani na Sita shawal (6).

Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) Ndg.Mohammed Ali Tedy amesema 8 bora ya ligi kuu ya Zanzibar inategemea  kuanza 14 july baada ya kumaliza kwa Michuano ya Kombe la Kagame, wameamua kufanya hivyo baada ya ushiriki wa JKU katika mashindano ya Kagame yanayo tarajiwa kuanza june 29 na kumaliza 13 jully.

Pia Tedy amesema baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani na sitatu shauwal (6) kumaliza wanategemea kuanza kwa kombe la FA ambalo zawadi zake zitatolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein. Michuano hiyo itakuwa kwa Kanda Mbili ya Unguja na Pemba

Mshindi kwa kila Kanda watapambana katika mchezo wa fainali na kupatikana mwakilishi wa Kombe la FA Cup 2018.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.