Habari za Punde

Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Wajumuika Katika Futari Maalum Ilioandaliwa na Balozi Seif Nyumbani Kwake Kama Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akijumuika pamoja na Viongozi na Wafanyakazi wa Ofisi yake katika futari ya pamoja iliyofanyika kwenye Makaazi yake Kama.
Baadhi na Viongozi na Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakijipatia vyakula kwenye futari ya pamoja iliyoandaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed akitoa neon la shukrani mara baada ya futari ya pamoja iliyofanyika nyumbani kwa Balozi Seif.(Picha na – OMPR )
Na.Othman Khamis OMPR.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Mh. Mohamed Aboud Mohamed amewapongeza na kuwashukuru Viongozi pamoja na Watendaji wa Ofisi hiyo kwa kazi kubwa waliyofanya iliyowezesha kufanikisha kupita kwa Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka 2018/2019 kwenye Kikao vya Baraza la Wawakilishi kinachoendelea.
Waziri Aboud kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alitoa pongezi hizo mara baada ya Viongozi na Watendaji hao kufutari pamoja katika Makaazi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi yaliyopo Kama nje kidogo ya Kaskazini ya Mji wa Zanzibar.
Alisema Bajeti ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha wa 2018/2019 haikuwa  na vikwazo vikubwa ikilinganishwa na Bajeti zilizopita kitendo ambacho kimedhihirisha umakini na ushupavu walionao Viongozi na Watendaji hao.
Waziri Aboud alifahamisha kwamba malezi ya Kazi waliyoyapata watendaji hao kupitia kwa Viongozi wao Wakuu  yamewawezesha kufanya kazi Kizalendo, wakizingatia moyo wa huruma sambamba na kupendana miongoni mwao na hatimae kupata mafanikio makubwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.