Habari za Punde

Balozi Seif mgeni rasmin katika Tamasha la Mashindano ya Shirikisho la Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar {Zahilfe}

  Baadhi ya Wanafunzi wa Shirikisho la Vyuo Vikuu na Taasisi ya Elimu ya Juu Zanzibar wakishiriki maandamano ya uzinduzi wa Tamasha la mashindano ya Shirikisho hilo kwenye Uwanja wa  Amani Mjini Zanzibar.
 Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar {ZAHILFE} Abdulatif Qadir Mussa akisoma Risala kwenye uzinduzi wa Tamasha la Mashindano ya Shirikisho hilo.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  wa kwanza Kulia akiwa na Waziri wa Elimu Riziki Pembe Juma na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Zahilfe Ayoub Mohamed Mahmoud wakishuhudia mashindano ya Riadha yaliyoandaliwa na Shirikisho la Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Zahilfe  ambae pia ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud akitoa salamu kwenye uzinduzi wa Tamasha la Mashindano ya Zahilfe hapo uwanja wa Aman
 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Riziki Pembe Juma akijiandaa kumkaribisha Balozi Seif  kulizindua Tamasha  la Mashindano ya Zahilfe kwenye uwanja wa Amani Mjini Zanzibar.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  akilizindua Tamasha  la Mashindano ya Shirikisho la Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar {Zahilfe}  kwenye uwanja wa Amani Mjini Zanzibar.

 Balozi Seif na Viongozi wenzake wakiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Soka ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar {SUZA} kabla ya kuanza pambano lao na Timu ya Soka ya Chuo Kikuu cha Sumait cha Chukwani.
 Balozi Seif na Viongozi wenzake wakiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Soka ya Chuo Kikuu cha Sumait cha Chukwani kabla ya kuanza pambano lao na Timu ya Soka ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar {SUZA}
 Timu za Soka za Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar {SUZA} na Chuo Kikuu cha Sumait kilipo Chukwani wakisimama kuwakumbuka  wanachama wenzao ambao tayari wameshafika mbele ya Haki{kufariki dunia}.
 Balozi Seif na Viongozi wenzake wakijumika pamoja na Wanachama wa Zahilfe wakisimama kuwakumbuka  wanachama wa Shirikisho hilo ambao tayari wameshafika mbele ya Haki{kufariki dunia}.
Picha na – OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.