Habari za Punde

JUMIA YARAHISISHA MANUNUZI SABA SABA JIJINI DAR ES SALAAM


Na Jumia Tanzania
Wateja wanaoshiriki katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Kibiashara ya Sabasaba mwaka 2018 wamerahisishiwa kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao na kupelekewa bidhaa zao mpaka wanapoishi.

Imezoeleka kwa kawaida wateja wanapokwenda kufanya manunuzi Sabasaba huwalazimu kubeba bidhaa zao. Jambo ambalo si tu huwasababishia usumbufu wa kubeba mizigo mingi, bali pia huwagharimu pesa kwa kulipia usafiri pamoja na kuhatarisha usalama wa bidhaa zao.  
Safari hii mambo yamekuwa tofauti kwani Jumia imetambulisha utaratibu mpya wa kufanya manunuzi kwa wateja ambao ni salama na rahisi zaidi kuutumia.

Utaratibu wa siku zote uliozoeleka ni kwa wateja kutembelea kwenye mabanda ya wafanyabiashara na makampuni tofauti ili kufanya manunuzi kwa bidhaa wanazoziona. Hii ni kwa sababu utamaduni wa Watanzania wengi wanapofanya manunuzi mbalimbali lazima waione bidhaa yenyewe ikiwezekana kuishika, kuikagua na wengine huenda mbele zaidi hata kwa kuijaribisha ili kujiridhisha zaidi.

Sababu kubwa kwa wateja wengi nchini na Afrika kwa ujumla kufanya hivyo ni kutokana na mfumo huu kuwa mgeni, masuala ya kiusalama hususani utapeli wa mitandaoni pamoja na changamoto ya teknolojia ambapo ni maeneo machache wanayoweza kunufaika.

Inachokifanya Jumia ni sawasawa na kusema maonyesho ya Sabasaba yaliyo kwenye mfumo wa mtandaoni. Kama unavyoona mabanda ya wafanyabiashara na makampuni tofauti kwenye maonyesho, Jumia nayo imesheheni bidhaa halisi na bora kutoka kwa maelfu ya wafanyabiashara tofuati nchini. Kwa kuzisajili biashara zao kwenye mtandao wake, wateja wanaweza kupata taarifa zote za bidhaa wanazozihitaji.
Kupitia mtandao wao, wateja wanaweza kuperuzi bidhaa za wafanyabiashara mbalimbali kama wanavyotembelea mabanda ya Sabasaba. Wateja wanaweza kuona bidhaa, maelezo yake, bei na kununua papo hapo na kisha kupelekewa mpaka alipo. Faida kubwa wanayojipatia kupitia mfumo huu ni kwamba malipo ya manunuzi yote hufanyika pale bidhaa zinapowafikia.

Wateja waliotembelea na wanaoendelea kutembelea Sabasaba watakuwa wamepata kitu kipya kwamba kwa dunia tunayoishi sasa unaweza kufanya manunuzi na kisha usionekane ukiwa umebeba mzigo wowote.

Katika msimu huu ambao Jumia inasherehekea miaka 6 ya huduma zake barani Afrika, wametoa ofa kemkem ikiwemo huduma ya bure ya usafiri. Hii itakuwa ni kwa wateja watakaonunua bidhaa za kuanzia shilingi 100,000 na kuendelea.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.