Habari za Punde

Tetesi za Soka Ulaya.: Willian na Barcelona, Mourinho, Fekir na Mina

Chelsea wanatafakari iwapo wakubali kumuuza kiungo wao wa kati Mbrazil Willian kwa £65m kwa Barcelona, huku taarifa zikidokeza kwamba Manchester United pia wanataka sana kumnunua mchezaji huyo wa miaka 29. (Mail)
Klabu hiyo ya Stamford Bridge inadaiwa pia kuwa katika juhudi za kutafuta eneo salama uwanjani ambapo kocha wao mpya Maurizio Sarri, 58, anaweza kuwa akivutia sigara hata siku ya mechi. Sarri ni mvutaji sugu wa sigara. (Mirror)
Chelsea pia wanaaminika kuwa bado na matamanio ya kumnunua mshambuliaji Mfaransa anayechezea Manchester United Anthony Martial, 22. (Talksport)
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anatarajiwa kukutana na makamu mwenyekiti mtendaji wa klabu hiyo Ed Woodward kujadiliana kuhusu wachezaji watakaonunuliwa au kuuzwa na klabu hiyo. (Express)
Beki wa Argentina Marcos Rojo, 28, ndiye mchezaji anayetarajiwa na wengi kuoneshwa lango ikiwa United watafanikiwa kumnunua beki wa England Harry Maguire, 25, kutoka Leicester. (Mirror)
Harry MaguireHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionHarry Maguire
Uwezekano wa Liverpool kumnunua kiungo wa kati wa Lyon Nabil Fekir, 25, unaonekana kufifia baada ya madai kuibuka kwamba huenda kusiwe na maafikiano. (Express)
Hata hivyo, klabu hiyo ya Anfield inadaiwa kuwa kwenye mazungumzo na klabu ya Besiktas ya Uturuki kuhusu uwezekano wa kumchukua beki wa Croatia Domagoj Vida, 29. (Star)
Vida’s header in extra-time gives Croatia 2-1 leadHaki miliki ya pichaBBC SPORT
Image captionDomagoj Vida
Nahodha wa England Harry Kane alizomewa na mashabiki baada ya nyota huyo wa Spurs kushiriki katika shindano la mchezo wa gofu siku ya mwisho ya The Open mjini Carnoustie, Scotland. (Sun)
Kiungo wa kati Jack Grealish, 22, anatarajiwa kuwafahamisha wamiliki wapya wa Aston Villa kwamnba anataka kujiunga na Tottenham Hotspur na kufuata ndoto yake ya kutaka kucheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. (Telegraph)
Colombia's Yerry MinaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionYerry Mina
Beki wa Colombia anayechezea Barcelona Yerry Mina, 23, anakaribia kuhamia Ligi Kuu ya England, akitarajiwa sana kutua Everton. (Goal)
Meneja wa Everton Marco Silva amekataa kuzungumzia ununuzi wa winga Richarlison, akisema ni lazima aheshimu hali kwamba mchezaji huyo wa miaka 21 bado ni mchezaji wa Watford. (Liverpool Echo)
Juventus wanadaiwa kuwasilisha ofa ya €30m (£26.8m) kutaka kumchukua beki wa Brazil Alex Telles kutoka Porto, lakini klabu hiyo ya Ureno inasisitiza kwamba bei yake haiwezi kuwa chini ya €40m (£35.7m). (Football Italia)
Beki wa Ukraine anayechezea Manchester City Oleksandr Zinchenko, 21, amekiri kwamba hajui mustakabali wake katika mabingwa hao wa Ligi Kuu England. (Manchester Evening News)
Oleksandr ZinchenkoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionOleksandr Zinchenko
Meneja Rafa Benitez hatarajiwi kufufua mazungumzo kati yake na Newcastle United kuhusu kurefusha mkataba wake hadi dirisha la kuhama wachezaji lifungwe.
Sheffield United wamewasilisha ofa ya £5m kutaka kumchukua mshambuliaji wa Ipswich mwenye miaka 28 Martyn Waghorn. (Sheffield Star)
Meneja wa Aston Villa Steve Bruce amesema mshambuliaji Ross McCormack, 31, na beki Micah Richards, 30, ni miongoni mwa wachezaji wanaolipwa pesa nyngi zaidi katika klabu hiyo inayocheza ligi ya Championship na wanaidhoofisha klabu hiyo kifedha. (Birmingham Mail)

Bora kutoka Jumapili

Chelsea wamewaambia Real Madrid kuwa hawawezi kulazimishwa kumuuza kiungo wa kati raia wa Ubelgiji mwenye miaka 27 Eden Hazard - hata kwa kima cha pauni milioni 170. (Mirror)
Rais wa Napoli Aurelio de Laurentiis ameonya kuwa meneja wake wa zamani Maurizio Sarri, ambaye sasa anaisimamia Chelsea kuwa hakutakuwa tena na makubaliano kati ya vilabu hivyo viwili. (Goal)
United wako tayari kumuongezea mkataba Anthony Martial ambao utamwezesha mshambuliaji huyo mfaransa mwenye miaka 22 kubaki nao hadi mwaka 2020. (Mirror)
Kiungo wa kati raia wa Brazil Andreas Pereira, 22, amemuambia meneja wa Manchester United Mourinho kuwa yuko tayari kucheza wakati wowote anapohitajika (Manchester Evening News)
Arsenal wamepiga hatua kawenye amzunguzmoa ya kumsainia kipa wa Borussia Monchengladbach raia wa Uswizi. Yann Sommer, 29. (Express)

Giroud na Petr Cech wanatafutwa

Aliyekuwa mlinzi wa Chelsea na Aston Villa John Terry, 37, anaripotiwa kustaafu kutoka kandanda huku kituo cha Sky Sports kikitaka ajiunge nacho. (Mirror)
Roma wanataka kumsaini kipa wa Arsenal Petr Cech, 36 kuchukua mahala pake kipa aliyehamia Liverpool Alisson. (Sun)
Atletico Madrid wamezungumza na Chelsea kuhusu uwezekano wa kumsaini mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud, 31, kwa mkopo. (Sky Sports)
Meneja wa Newcastle, Rafa Benitez atapewa kitita cha pauni milioni 100 kununua wachezaji ikiwa atakubali mkataba mpya wa miaka mitatu. (Sun)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.