Habari za Punde

Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dkt. Khalid Atembelea Mradi wa ZSSF Jumba la Treni Darajani Leo.

Ujenzi wa Jumba la Treni Darajani Zanzibar likiendelea na Ujenzi wake unaofanywa na Kampuni kutoka China ya CRJE, likiwa katika hatua za mwisho ya ujenzi huo na kutarajiwa kufunguliwa hivi karibuni baada ya kukamilika kwa uwekaji wa miundombinu katika jengo hilo. Baada ya kukamilika Ukarabati wake mkubwa. 
Msimamizi wa Kampuni ya Ujenzi ya China ya CRJE Anthony Changali akitowa maelezo ya kiufundi kwa Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar Mhe. Dkt. Khalid Mohammed Salum wakati alipofanya ziara kukagua ujenzi huo na kuridhika kwa hatua iliofikia katika ujenzi huo mkubwa wa kulikarabati jengo hilo likiwa na Maduka, Mgaghawa, Sehemu ya Mazoezi na Nyumba za Kuishi.
Sehemu ya ghorofa ya kwanza ya jengo hilo la Jumba la Treni sehemu ya maduka na Ofisi kama inavyoonekana pichani sehemu hiyo.
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar kulia Mhe. Dkt. Khalid Mohammed Salum, akitembelea  sehemu za Maduka katika jengo la Jumba la Treni Darajani Zanzibar wakati wa ziara yake kutembelea Mradi huo ulioko chini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF, katikati Kaimu Meneja Miradi na Uwezeshaji ZSSF Ndg. Abdulazizi Abrahaman Iddi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa ZSSF Ndg. Khamis Filfil Thani akitowa maelezo kwa Waziri wa Fedha na Mipango wakati akitembelea jengo hilo wakati wa ziara yake leo.
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar kulia Mhe. Dkt. Khalid Mohammed Salum, akitembelea  sehemu za Maduka katika jengo la Jumba la Treni Darajani Zanzibar wakati wa ziara yake kutembelea Mradi huo ulioko chini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF, katikati Kaimu Meneja Miradi na Uwezeshaji ZSSF Ndg. Abdulazizi Abrahaman Iddi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa ZSSF Ndg. Khamis Filfil Thani akitowa maelezo kwa Waziri wa Fedha na Mipango wakati akitembelea jengo hilo wakati wa ziara yake leo.kushoto Meneja Mradi wa Kampuni ya CRJE Wu Haibo.
Sehemu ya Nyumba ya Jengo hilo la Jumba la Treni Darajani Zanzibar kama linavyoonekana picha kukamilika kwake ujenzi unaofanywa na Kampuni kutoka China ya CRJE.
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Dkt. Khalid Mohammed Salum akiwa katika ziara yake kukagua ujenzi wa jumba la treni darajani wakati wa ziara yake leo kujionea Mradi huo ukiwa katika hatua ya mwisho ya ujenzi wake unaofanywa na Kampuni ya CRJE kutoka Nchini China.
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Dkt. Khalid Mohammed Salum akizungumza wakati wa ziara yake kutembelea Miradi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF, kulia Kaimu Mkurugenzi Muendeshaji wa ZSSF Ndg. Khamnis Filfil Thani na  kushoto Menaja Mradi wa Kampuni ya CRJE Ndg. Wu Haibo wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar wakati wa ziara yake kutembelea mradi huo.
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. DktKhalid Mohammed Salum, akimsikiliza Mwakilishi wa Kampuni ya Kichina inayofunga AC kutoka kampuni ya CITCC Ndg. Eric Lin Zhijin, wakati alipotembelea eneo la kufungwa kwa mtambo huo wa AC katika eneo hilo la darajani kwa ajili ya kutumika katika jengo la Jumba la Treni Darajani. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.