Habari za Punde

Uchaguzi Zimbabwe: Nelson Chamisa Apinga Ushindi wa Rais Emmerson Mnangagwa

Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe amepinga ushindi wa Rais Emmerson Mnangagwa akisema matokeo yaliotolewa ni bandia.
Mnanganga alitangazwa mshindi kwa mara ya kwanza tangu kung'atuliwa kwa rais Robert Mugabe.
Chama cha Nelson Chamisa MDC Allkiance kimeapa kwenda mahakamani kupinga uchaguzi huo akisema kuwa kura hiyo ilifanyiwa udanganyifu.
Bwana Mnangagwa amewatalka raia wa Zimbabwe kuungana nyumba ya uongozi wake.
Maafisa wa polisi wanaendelea kupiga doria katika barabara za mji wa Harare baada ya maandamano kusababisha vifo vya watu sita.
Mwandishi wa BBC mjini humo anasema kuwa gari la polisi lililokuwa na kipaza sauti lilizunguka likisambaza ujumbe kwamba 'Zimbabwe iko wazi kwa biashara'.
''Tuko hapa kuwalinda .Jisikieni huru mutembee na kufungua biashara, kila kitu kiko shwari musiogope''.
Katika majimbo 10 yote yalioyotangazwa, Mnangagwa ameshinda kwa asilimia 50.8 ya kura kwa asilimia 44.3 alizopata mgombea wa chama cha upinzani Nelson Chamise.
Polisi waliwaondoa upinzani wakati wa kutangazwa matokeo baada ya kukataa kuyakubali matokeo hayo.
Hatahivyo Mwenyekiti wa chama cha MDC Alliance, Nelson Chamisa amesema kuhesabiwa kwa kura hakukufanyiwa uhakiki.
Kwa ushindi wa asilimia 50 wa Mnangagwa umesababisha aepuke kwenda duru ya pili ya uchaguzi dhidi ya Chamisa.
Rais Mnangagwa amesema katika ukurasa wake wa Twitter kuwa huu ni mwamzo mpya.
Bwana Chamisa amesisitiza kuwa ZANU-PF haikushinda uchaguzi huu, wanajaribu tuu kupitisha suala lisilo na ukweli, amesema pia watapambana na suala hilo.
Uchaguzi huu ulikuwa wa kwanza tangu kiongozi wa muda mrefu Robert Mugabe kung'atuliwa madarakani.
Wananchi wa Zimbabwe wakishangilia Ushindi baada ya kutangazwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Nchi hiyo. 


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.