Habari za Punde

Zura yaanzisha huduma kuwasaidia wanaokabiliwa na matatizo ya huduma ikiwemo Maji Umeme na Gesi.

Na Mwashungi  Tahir    Maelezo       

MAMLAKA Ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati ZURA Imeanzisha Baraza la Watumiaji la Zura ili kuweza kuwasaidia wananchi  wanaokabiliwa na matatizo ya huduma ikiwemo Maji Umeme na Gesi.
Hayo aliyasema huko kwenye Ofisi ya Zura iliopo Maisara  mwasilishaji Mwanasheria Mwandamizi ZURA  Rashid Abdullah Fadhil  alipokuwa akiwasilisha mada ya Baraza la Watumiaji  wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema Baraza la Watumiaji la Zura ni Baraza la Watumiaji wa Huduma zinazodhibitiwa  ambalo  limeanzishwa chini ya kifungu Nam 33 cha  sheria ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati ZURA  Nam 7.2013.

Akielezea lengo la kuanzishwa kwa baraza hilo  ni kutetea na kulinda maslahi ya watumiaji wa Huduma za Maji na Nishati  Umeme , Mafuta na Gesi kwa kuwa mtumiaji  anatumia huduma ya maji na Nishati mara kwa mara  au ameshawahi kutuma moja ya bidhaa zinazodhibitiwa na ZURA.

Aidha alisema kazi za Baraza la Watumiaji linatekeleza majukumu yake kisheria  kwa kutetea na kulinda maslahi ya watumiaji wa Huduma zinazidhibitiwa na Zura  kwa kufanya maamuzi , kutoa maoni na taarifa   pamoja na kushauriana na Mamlaka , pamoja na Wizara husika.

Pia alisema kazi nyengine ya Baraza hilo ni kupokea na kusambaza taarifa kuhusu maslahi ya watumiaji wa Huduma zinazodhibitiwa na Zura  na pia kushauriana na wenye viwanda vikubwa , Serikali  na vikundi vya watumiaji vya sekta zinazodhibitiwa.

Akifafanua kuhusu njia za kuwasilisha malalamiko alisema baada ya kufuata taratibu zote za kuwasilisha malalamiko mtumiaji atatakiwa kuwasilisha malamamiko moja kwa moja kwenye kitengo cha huduma kwa Wateja  cha mtoa Huduma wake.

Vile vile alisema endapo malalamiko yake hayatofanyiwa kazi , mlalamikaji anapaswa kuwasilisha malalamiko yake ZURA , akipeleka nakala ya barua ya malalamiko kwa Baraza la Watumiaji kumuwezesha kufuatilia maendeleo ya shauri husika.

Nae Kaimu Mkuu wa Kitengo cha  uhusiano wa Mamlaka yaUdhibiti wa Huduma ya Maji na Nishati ZURA  Khuzaimat Bakar Kheir aliwataka wananchi  walitumie baraza hilo ili kuweza kutatua migogoro yao kwa kupitia mpango maalum .

Pia alisema elimu itaendelea kutolewa kwa wananchi ili waweze kufaidika na baraza hilo ambalo liko kwa ajili ya kutatua changamoto za wananchi katika utumiaji wa huduma hizo.

Sheria yaZURA kwa kupitia kifungu cha 33 kkimefafanua uteuzi wa wajumbe wa Baraza la Watumiaji linatakiwa liwe na Wajumbe wasiopungua watano  (5) na wasiozidi saba(7) ambao wajumbe hao wanatokana na Taasisi zisizo  za Kiserikali ambazo zinatambulika kisheria hapa Zanzibar ambao watateuliwa na Waziri anayeshughulikia ZURA.
Mwisho.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.