Habari za Punde

Kituo cha Online Tv cha Al Fatah TV Online Zanzibar Chakabidhia Leseni ya Utangazi Kupitia Mitandaoni na Tume ya Utangazaji Zanzibar.

Mrajisi wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Ndg. Omar Said Ameir akimkabidhi leseni ya Utangazaji kupitia Mtandaoni Online Tv Mkurugenzi Mkuu wa Al Fatah Online Tv Ndg. Rashid Salum Mohammed, baada ya kukamilisha taratibu zote za usajili kupitia Tume ya Utangazaji Zanzibar baada ya kutolewa Tamko kwa Kila TV Online na Blog kufanyiwa Usajili ili kuweza kutambuliwa na Serikali ufanyaka kazi wao uwe kihalali, akishuhudia Mhandisi wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Eng. Ali Ayoub Hussein, hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za Tume hiyo Kikwajuni Zanzibar.
 Mrajisi wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Ndg. Omar Said Ameir akitowa maelezo ya kanuni za Sheria za Matumizi ya Utangazaji kupitia Online Tv kwa Mmiliki wa Kituo cha Tv Online cha Al Fatah Online Tv Rashid Salum Mohammed, Makao Makuu yake yako Maungani Zanzibar.

1 comment:

  1. Mimi nataka kufahamu ni vigezo gani ili uweze kupata leseni hio

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.