Habari za Punde

Taasisi ya Milele yakabidhi msaada wa vitabu vya kiingereza kisiwani Pemba

 Meneja wa Taasisi ya Milele Zanzibar  Foundation, Abdalla Saidi Abdalla, akizungumza machache mikakati iliojiwekea taasisi hiyo katika kukuza huduma za elimu nchini hususan kwa somo la Kingereza.
 Walimu wakuu wa Skuli teule na maafisa Elimu Wilaya na Mikoa na Waratibu wa vituo vya Elimu masafa TC Pemba ,wakiwaka katika mkutano wa hafla ya makabidhiano ya Vitabu vya kusomea Kingereza vilivyotolewa na taasisi ya Milele Zanzibar Foundation huko Mfikiwa Pemba.
 Ofisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya amali Zanzibar, Maalimu, Mohammed Nassor Salim, akiwahutubia Walimu wa Skuli teule zilizopatiwa msaada wa Vitabu vya kusomea somo la Kingereza pamoja na maafisa mbali mbali wa Elimu Kisiwani juu ya matumizi ya Vitabu hivyo katika hafla iliofanyika huko katika Ofisi ya taasisi hiyo Mfikiwa Wawi Pemba.

Ofisa mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya amali Pemba , akimkabidhi Mwalimu  mkuu wa Skuli ya Birikau katika Wilaya ya Chake Chake Pemba, kwa niaba ya walimu wenzake wa Skuli teule zilizopatiwa msaada wa vitabu vya kusomea Kingereza vilivyotolewa na taasisi ya Milele Zanzibar Foundation. PEMBA.


PICHA NA HABIBA ZARALI -PEMBA.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.