Habari za Punde

Uvuvi wa Samaki Aina ya Kambare Katika Bwawa la Mwanakwerekwe Zanzibar Baada ya Kupungua Maji Katika Bwawa Hilo Huleta Nema Kwa Wananchi.

Wananchi katika eneo la mwanakwerekwe Zanzibar wakivuatilia Vijana wakiwa katika bwawa la mwanakwerekwe wakivua Samaki aina ya Kambare katika bwawa hilo baada ya kupungua kima cha maji yanayotokana na kunyesha kwa mvua za masaki zilizomaliza hivi karibuni.
Bwawa hilo hujaa maji na kufurika mpaka katika barabara inayokatisha katika bwawa hilo kuelekea fuoni na njia ya Kusini Unguja.

Vijana hao wakitumia nyavu za kuvulia samaki wakiwatega samaki hao aina ya kambere baada ya kupungua maji katika bwawa hilo. kama walivyokutwa wakiwa katika zoezi hilo likiendelea la uvuvi huo. na kuuza kwa shilingi 8000/= mpaka shs.10,000/= inategemea ukubwa wake.
Zoezi la uvuaji wa Samaki aina ya kambare likiendelea katika bwawa hilo kama wanavyoonekana wakiwa katika zoezi hilo na nyavu zao wakiwatega.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.