Habari za Punde

Uzinduzi wa Tamasha la Kwanza la Hifadhi ya Urithi wa Mtanzania Kuzinduliwa Viwanja Vya Maisara Zanzibar Tarehe 24 Hadi 29 Septemba 2018.

Naibu Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Chuom Kombo Khamis akizungumza na Waandishi wa habari wa Vyombo vya Serikali na Binafsi kuhusiana na kukamilika kwa Maandalizi ya Maonesho ya Tamasaha la Kwanza la Urithi Mtanzania litakalofanyika katika viwanja vya mpira maisara Zanzibar na kushirikisha Wasanii na Vitu vya Asili kutoka Unguja na Pemba. Tamasha hilo litafanyika kuazia tarehe 24/9/2018 na kufikia tamati ya tamasha hilo tarehe 29/9/2018. 
Naibu Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Choum Kombo Khamis akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa Tamasha la Kwanza la Urithi wa Mtanzania katika Viwanja vya Maisara Zanzibar, mkutano huo umefanyika katika ukumbi mdogo wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.

Waandishi wakifuatilia mkutano huo na Naibu Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar kuhusiana na Uzinduzi wa Tamasha la Kwanza Zanzibar la Urithi wa Mtanzania katika viwanja vya maisara Zanzibar.
Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Dkt. Juma Mohammed Salum akizungumza baada ya mkutano huo kumalizika uliofanyika ukumbi mdogo wa mikutano wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.