Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mgeni wake Mtawala wa Nchi ya Ras Al Khaimah Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasim, alipowasili katika viwanja vya Ikulu Zanzibar kuhudhuria Utiaji wa Saini ya Mkataba wa Makubaliano ya Uzalishaji wa Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar na Kampuni ya RAKGAS ya Ras Al Khaimah. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na mgeni wake Mtawala wa Nchi ya Ras Al Khaimah Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasim, wakiwa wamesimama wakati walipowasili katika viwanja vya Ikulu kwa ajili ya kuhudhuria hafla hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Mgeni wake Mtawala wa Ras Al Khaimah Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasim, wakifuatilia maelezo ya kitaalam ikitolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Maji Nishati na Makaazi Zanzibar Ndg Ali Halil Mirza wakati wa hafla hiyo ya Utiaji wa Saini ya Mkataba wa Makubaliano ya Uzalishaji wa Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar. 
Balozi wa UAE Nchini Tanzania Balozi Mohammed Al Hammad, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi wakifuatilia hafla hiyo katika viwanja vya Ikulu Zanzibar. No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.