Habari za Punde

Mbunge wa Viti Maalum CCM Mhe. Rose Tweve Azindua Mfuko wa Maendeleo wa UWT Iringa Vijijini.

Mbunge wa viti maalum kupitia chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa Rose Tweve akiwa na   umoja wa wanawake (UWT) wilaya ya Iringa vijijini ambao wamefanikiwa kuunda mfuko wa maendeleo kwa ajili ya kukuza kipatao chao. 
Mbunge wa viti maalum kupitia chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa Rose Tweve akiangalia vitu vilivyotengenezwa na akinamama ambao tayari amewawezesha
MBUNGE wa viti maalum kupitia chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa Rose Tweve akiongea na umoja wa wanawake (UWT) wilaya ya Mufindi

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
MBUNGE wa viti maalum kupitia chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa Rose Tweve amefanikiwa kuunda mfuko wa umoja wa wanawake (UWT) wilaya ya Iringa vijijini ambao utasaidia kukuza kipata na kuongeza kasi ya maendeleo.

Akizungumza na blog hii mbunge huyo alisema kuwa amefanikiwa kufanya ziara katika wilaya Iringa vijijini na kuziwezesha kata zote kwa kutoa shilingi laki sita kwa kila kata.

“Nimetembea kata ishirini na nane (28) na kutoa shilingi 600,000 kwa kila kata kwa wanawake wa UWT ili kukuza uchumi wa jumuiya hiyo ambayo ndio imekuwa nguzo kwa familia yoyote ile” alisema Tweve

Tweve alisema kuwa tayari amezunguka katika kata zote 36 za wilaya ya Mufindi na kufanikiwa kuwawezesha kama alivyo fanya kwenye wilaya ya Iringa vijijini hivyo anajipanga na kuhakikisha kote huko wanaunda mfuko wa wilaya kwa maendeleo ya wanawake hao.

“Mimi ni mbunge ambaye nimechaguliwa na wanawake wa chama cha mapinduzi hivyo ni lazima nihakikishe nawaletea maendeleo kwa kutumia ubunifu wangu wote na kuhakikisha wananchi wanaunga mkono juhudi za Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli” alisema Tweve

Aidha Tweve alisema kuwa lengo ni kuhakikisha anazifikia kata zote za mkoa wa Iringa na kuwawezesha akinamama kiuchumi ili kufanya maendeleo kwa kuendana na kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli

“Hadi sasa nimefanikiwa kutoa zaidi ys shilingi milioni 38,400,000 kwa ajili ya kuwawezesha wanawake wa mkoa wa Iringa ili waweze kukuza vipato vyao vya kiuchumi” alisema Tweve

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.