Habari za Punde

Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Atembelea Mradi wa Ujenzi wa Skuli ya Msingi Kiombamvua.

 Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi akifanya ziara fupi ya kulikagua Jengo Jipya la Madarasa Manne ya Skuli ya Msingi Kiombamvua.
Balozi Seif  akiueleza Uongozi wa Kamati ya Skuli ya Msingi Kiombamvua nia yake ya kukamilisha ahadi yake ya Mchango wa Matofali 500 zilizobakia kati ya 1,000 kuendeleza Ujenzi wa Jengo Jipya la Skuli hiyo.
Kulia ya Balozi Seif ni Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Msiunginya Kiombamvua Mwalimu Jecha Songoro Kinole na Mbunge wa Jimbo la Mahonda Mheshimiwa Bahati Abeid Nassir.
Balozi Seif akitembelea Madarasa ya Kwanza nay a Pili ya Skuli ya Msingi ya Kiombamvua baada ya kukagua Ujenzi wa Jengo jengine jipya lililoanza kujengwa la Skuli hiyo.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Na.Othman Khamis OMPR.
Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi aliwakumbusha Wananchi kuzingatia umuhimu wa kubuni na hatimae kuanzisha miradi yao ya Maendeleo na Kijamii ili iendelee kuleta ustawi wa hatma yao njema ya sasa na hapo baadae.
Alisema hatua hiyo itajenga nguvu za pamoja zitakazohamasisha Viongozi wao wa Jimbo, Serikali pamoja na wahisani wa ndani na nje ya Nchi kuunga mkono jitihada za Wananchi hao katika kuanzisha miradi hiyo.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa kumbusho hilo wakati alipofanya ziara fupi ya kulikagua Jengo la Madarasa Manne la Skuli ya Msingi ya Kiombamvua akijiandaa ndani ya Wiki hii kukamilisha ahadi aliyotoa ya kumaliza mchango wa Matofali 500 kati ya 1,000 wakati alipohamasisha kujengwa kwa jengo hilo.
Alisema ipo miradi kadhaa inayoanzishwa na Wananchi wenyewe kwenye Shehia na Majimbo ambayo baadae hupata msukumo wa haraka kutokana na uzito wa miradi inayohusika.
Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza Wananchi wa Shehia ya Kiombamvua kwa ubunifu wao wa kuongeza Majengo ya Madarasa ili kuwaondoshea usumbufu Watoto wao kufuata Elimu masafa marefu ambayo pia huambatana na kuwaepusha na hatari ya matumizi ya bara bara.
Naye kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mahonda Mheshimiwa Bahati Abeid Nassir aliahidi kuchangia Saruji itakayokidhi mahitaji ya Ujenzi wa Jengo hilo la Madarasa Manne mpaka hatua ya kukabidhiwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya  Amali kwa ajili ya ukamilishwaji.
Hata hivyo Mh. Bahati alisema kwa mujibu wa makubaliano na Kamati ya Uongozi wa Skuli hiyo awamu ya kwanza ya ujenzi huo itazingatia kukamilisha  Madarasa Mawili ili yakidhi mahitaji ya kuhudumia Wanafunzi wa Darasa ya Pili wa Skuli hiyo wanaotarajiwa kuingia Darasa la Tatu hapo Mwakani.
Mapema Uongozi wa Kamati ya Skuli ya Msingi ya Kiombamvua uliwaeleza Viongozi hao wa Jimbo kwamba ujenzi wa Jengo hilo Jipya la Madarasa Manne umekisiwa kugharimu jumla ya shilingi Milioni 18,000,000/- hadi kukamilika kwa hatua ya Linta.
Walisema Awamu ya Kwanza ya Ujenzi wa Jengo hilo kwa lengo la kuwahi Madarasa Mawili kwa sasa umepangwa kugharimu Shilingi za Kitanzania Milioni 7,200,000/-.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.