Habari za Punde

Tume ya Utangazaji Zanzibar (ZBC) Yakabidhi Leseni ya Kituo Cha Utangazaji Cha Tv Kijulikanacho Kwa Jina la Mambo TV Swahili.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Mr. Chande Omar akimkabidhi leseni ya Utangazaji kupiotia Online TV Mmiliki wa Kituo cha Television cha Mambo TV Swahili Ndg. Adil Ally Saleh, hafla hiyo ya kukabidhi leseni hiyo zimefanyika katika Ofisi za Tume Kikwajuni Zanzibar, akishuhudia Mrajisi wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Ndg. Omar Said Ameir.
Mmiliki wa Kituo cha TV cha Mambo TV Swahili Ndg. Adil Ally Saleh akionesha Leseni yake baada ya kukabidhiwa na Kaimu Murugenzi Mtendaji wa Tume Ndg. Chande Omar, hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za Tume ya Utangazaji Kikwajuni Zanzibar. 
Mrajisi wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Ndg. Omar Said Ameir, akimkabidhi leseni Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Chande Omar, kwa ajili ya kumkabidhi Mmiliki wa Kituo cha  TV cha Mambo TV Swahili yenye makazi yake welesi Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.