Habari za Punde

Kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar.


Na Mwashungi Tahir .Maelezo Zanzibar.
Kamati ya Fedha , Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi , kuhusu mswada wa sheria ya kufuta sheria ya ukuzaji na kulinda vitega uchumi Zanzibar nam, 11 ya mwaka 2004 na kutunga sheria ya mamlaka ya ukuzaji na kulinda vitega uchumi Zanzibar na kuweka masharti mengine yanayohusiana na hayo.
Hayo ameyasema Mwenyekiti wa kamati hiyo Dkt Mwinyihaji Makame  huko katika ukumbi wa  baraza la Wawakilishi Chukwani nje kidogo ya mji  wa Zanzibar wakati alipokuwa  akiwasilisha mswaada wa sheria  hiyo kwa Wawakilishi wa Baraza hilo.
Alisema Ofisi ya Baraza la wawakilishi kwa kuanzisha utaratibu wa kutupatia dozi nzuri ya mafunzo ambayo kwa kiasi kikubwa yuameweza kutupa mwangaza wa kile kilokusudiwa kuelezwa  kisheria ndani ya mswaada huo.
Pia alisema Kamati hiyo inaipongeza Serikali kwa kuleta mswada huo katika wakati muafaka ambapo nchi imo kwenye mageuzi ya kiuchumi kutoka uchumi wa kutegemea kilimo hadi uchumi wa viwanda kupitia wawekezaji tofauti , katika uchambuzi wa  mswada ulioletwa kamati imegundua kasoro ndogo ndogo na kufanya marekebisho kwa nia ya kuimarisha zaidi.
Akielezea maeneo yaliyofanyiwa marekebisho ya uanzishwaji wa kitengo maalum cha kutoa huduma kwa wawekezaji ambapo wakati wa kupitia na kujadili mswada huo . Kamati ilifarijika sana kuona kilio chake cha siku nyingi cha kuanzishwa kitengo hicho maalum cha kutoa huduma kwa Wawekezaji na wafanyabiashara kwa ujumla kimepatiwa ufumbuzi.
Alisema Mwenyekiti huyo kwa kipindi kirefu kamati ilikuwa ikihimiza sana juu ya uanzishwaji wa kitengo hicho kupitia ziara zake mbali mbali ilizokuwa ikizifanya , ni dhahiri kuwa uanzishwaji wa kituo hicho “One Stop Centre”utarahisisha  upatikanaji wa huduma kwa wawekezaji wa ndani nan je ya Nchi kuongeza ajira kwa vijana kupitia sekta mbali mbali pamoja na kuinua pato la Taifa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.