Habari za Punde

MAJALIWA AKUTANA NA MAWAZIRI ENEO LA IHUMWA DODOMA UNAPOJENGWA MJI WA SERIKALI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako wakati alipowasili kwenye eneo la Ihumwa jijini Dodoma, unapojengwa Mji wa Serikali kukutana na Mawaziri na Makatibu Wakuu, Desemba 28, 2018. Wengine pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI, Selemani Jafo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Augustine  Mahiga, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango na kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mawaziri na Makatibu Wakuu kwenye eneo la Ihumwa jijini  Dodoma unapojengwa mji wa Serikali
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dkt. Maulid Banyani baada ya kuzungumza na Mawaziri na Makatibu Wakuu kwenye eneo la Ihumwa jijini Dodoma unapojengwa Mji wa Serikali, Desemba 28, 2018.  Katikati ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi baada ya kuzungumza na Mawaziri na Makatibu Wakuu kwenye eneo la Ihumwa jijini Dodoma unapojengwa mji wa serikali, Desemba 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.